Aina kuu mbili za elimu zitakazo kusaidia kufanikiwa Sana kwenye dunia ya sasa.

Moja Kati ya nyenzo muhimu Sana ya mafanikio katika dunia yoyote Ile ni elimu.

Nchi zilizoendelea hasa zile zinazojiita nchi za ulimwengu wa kwanza ziliijua Siri hii mapema Sana na kuamua kuwekeza nguvu zao zote katika kuwa elimisha watu wao na elimu waliyoipata ndiyo imewaletea Maendeleo na mafanikio makubwa waliyonayo sasa.

Kwa upekee wa nyenzo hii, kampeni nyingi Sana ziliendeshwa duniani kote, kila nchi inaweka kipaumbele sana katika elimu ya watu wake ili waelimike na kuweza kuwa watatuzi wa changamoto mbalimbali zinazowakabili na kuleta Maendeleo.

licha ya uzuri na manufaa yote ambayo elimu imekuwa nayo, bado wananchi wengi wa nchi nyingi zinazoendelea hasa zile za ulimwengu wa tatu wanaona kama elimu waliyoipata siyo mkombozi wa changamoto zao, hii imetokana kuwa aina ya elimu ambayo watu wameipata haikulenga Sana kuwafanya wao kuwa na umahili ambao ungeweza kuwa sehemu ya majibu na ufumbuzi wa changamoto za maisha Yao na badala yake imewafanya wasomi wengi kuwa tegemezi.

Jambo hili limetokea kwa sababu mfumo mzima wa elimu umekuwa una waandaa watu kwa lengo la kwenda kuajiriwa kufanya Kazi kwenye taasisi na mashirika mbalimbali ya kiserikali na Yale ya watu binafsi na siyo kwa lengo la kuitumia elimu waliyopata kwa ajili ya kuwezesha ustawi wa maisha yao na kuwa na uwezo wa kujitegemea.

Hapa ndipo unapokutana na zile Imani kwamba mwanangu nenda shule, kasome kwa bidii, faulu mitihani yako vzuri ili uweze kupata Kazi nzuri itakayokusaidia kuweza kuwa na maisha mazuri.

Imani hizi zimetumiwa Sana na wazazi na bado zinatumiwa Sana hata sasa kuwasisitiza wanafunzi kusoma kwa bidii wakiamini kuwa mtu akisoma atapata Kazi nzuri ambayo itamwezesha kuwa na maisha bora.

lakini sasa kwa dunia tuliyonayo wakati huu Imani hii imegeuka kuwa uongo. Yaani swala la kusoma ili uwe na uhakika wa kupata Kazi kwa sasa imekuwa ni uongo kabisa na haifanyi Kazi kama ilivyokuwa zamani.

Dunia ya sasa haitaki mtu kuwa na elimu tu ya darasani inayo kufundisha kusoma, kuandika, kuhesabu na kuandaliwa kuwa mtu fulani baadae hapana. Dunia ya sasa inataka uwe na elimu inayoendana na Kasi ya mabadiliko na inayokuwezesha kuweza kutatua changamoto mbalimbali za maisha yako.

sasa kwa miaka mingi watu wamekuwa wanajifunza na kufundishwa aina mbili tu za elimu huko mashuleni.

aina ya kwanza ni elimu ya msingi ya mfumo rasmi.

aina hii ya elimu ndo Ile iliyokufundisha kusoma, kuandika, kuhesabu na kujua aina mbalimbali ya vitu. Hii ni elimu ya msingi Sana uliyopata na Ina msaada Sana kwenye maisha yako kwani ndiyo imekupa uwezo wa wewe kuweza kuhusiana na mazingira yako sawasawa licha ya kuwa kwa sasa aina hii ya elimu bado haitoshi kwa wewe kuweza kufanikiwa kwa viwango vya juu sana katika dunia hii tuliyonayo.

Aina ya pili ya elimu ambayo pia umefundishwa huko shuleni hi hii elimu ya taaluma flani. wazungu wanaiita (professional education)

katika elimu hii ndipo wataalamu mbalimbali wamekuwa wanaandaliwa kwa ajili ya kuweza kufanya Kazi mbalimbali zinazoendana na masomo waliyosomea.

hapa ndipo utakutana na watu wanaoitwa mawakili wasomi, wana sheria, wahasibu, walimu, wahandisi, madaktari, wana uchumi, na majina mengine mengi yanayohusu taaluma.

Aina hii ya pili ya elimu ni ya msingi Sana pia kuwa nayo kwani ndiyo imewezesha watu kufanya Kazi kwenye maeneo mbalimbali na kuweza kuleta Maendeleo kwa wao binafsi na familia zao, Maendeleo katika jamii na nchi kwa ujumla. Lakini kwa dunia ya sasa bado elimu hii pekee haitoshi kwa wewe kuweza kufanikiwa Sana.

Hii ni kutokana kuwa msingi wa mfumo huu wa elimu ni tegemezi na umekuwa na lengo la kumuandaa mtu kwa ajili ya kuajiriwa.

Pia kumekuwa na mapokeo yasiyo sahihi ya wasomi kupambana na mitihani ili kuwa na ufahulu mzuri utakao wawezesha kupata Kazi na kuacha kutilia Makazo Sana kwenye kujenga uwezo na uelewa utakaowawezesha kuendesha maisha yao

Sasa pamoja na watu kupata aina izo mbili za elimu bado wengi wanaendelea kukubwa na changamoto maishani mwao.

Yaani elimu izo zimeshindwa kuwa msaada na watu wengi wameingia katika majuto, malalamiko na utegemezi ulio kisiri.

Kwa kupitia Makala hii naomba nikufundishe aina nyingine mbili za elimu ambazo unaziitaji na zitakusaidia Sana kwa dunia ya sasa. Aina izi za elimu licha ya kuwa zinafanya Kazi kubwa na zimewasaidia watu wengi kufanikiwa bado hazifundishwi mashuleni

Aina ya kwanza ya elimu isiyofundishwa shuleni ni ELIMU YA MSINGI YA FEDHA.

licha ya kuwa maisha yetu yanategemea Sana pesa ili yaweze kwenda sawasawa, elimu ya msingi ya fedha bado haitolewi Wala haifundishwi mashuleni.

yaani hakuna sehemu kwenye mitaala ya elimu inayotufundisha namna ya kuingiza pesa, namna ya kutumia pesa, namna ya kudhibiti pesa, namna ya kutunza pesa, namna ya kuzalisha pesa zaidi Wala namna ya kuwekeza pesa.

na hata kama mtu amesoma kozi zinazohusu maswala ya pesa bado alichojifunza siyo kwa lengo la yeye binafsi ameandaliwa kwa ajili ya kufanya Kazi kwenye taasisi za kifedha.

na ndiyo maana utakuta mtu ni muhasibu wa kampuni au shirika flani na anafanya vzuri kutunza na kusimamia pesa za kampuni ilo lakini anashindwa kusimamia pesa zake binafsi.

ili ni kosa kubwa Sana ambalo lina kwamisha Maendeleo ya watu wengi kwenye maisha yao.

Tunaweza kupata pesa kwa njia mbalimbali tunazozijua lakini atujafundishwa nguvu ya pesa na namna ya kuitumia sawasawa, hatujui kuhusu kuweka bajeti, hatujui kuhusu umuhimu wa akiba, atujui namna ya kuizalisha pesa zaidi na bado hatujui kabisa kuhusu uwekezaji.

ivyo kama utataka kufanikiwa zaidi kwenye maisha yako anza kuwekeza katika kutafuta elimu hii muhimu na utafanikiwa Sana.

Kupata aina hii ya elimu inakubidi utumie jitihada zako kujifunza kupitia kusoma vitabu mbalimbali vya fedha, kuhudhuria semina zanazoelezea kuhusu fedha na sikiliza na kuangalia video mbalimbali zinazoeleza kuhusu fedha kwa kufanya ivyo utakuwa Bora zaidi na utaweza kufikia mafanikio yako.

Aina ya pili ya elimu isiyofundishwa shuleni ni ELIMU JUU YA MAENDELEO BINAFSI.Wazungu wanaiita ( self development education)

Aina hii ya elimu imewasaidia watu wengi sana na inaendelea kuwa mkombozi na msaada mkubwa Sana kwa watu wengi hasa kwenye dunia tuliyonayo sasa ambayo inabadilika kila siku.

Elimu ya Maendeleo Binafsi ndiyo itakayokusaidia wewe kujua kusudi la maisha yako, kwa nini upo hapa duniani na unatakiwa kufanya nini

elimi hii inakupa uwezo wa kujua uwezo, karama na vipaji ulivyo navyo na jinsi ya kuvitumia ili kuleta matokeo chanya katika maisha yako.

pia kupitia elimu hii utaweza kujenga tabia zitakazo kuletea mafanikio makubwa Sana, tabia kama kuweka malengo na kuya simamia, kuwa na mtazamo chanya juu ya maisha yako, jinsi ya kutumia muda na kuheshimu rasilimali zako nyingine ambazo ni muhimu mfano fedha na Mali.

Lakini pia utaweza kujua jinsi ya kulinda na kujali afya yako, jinsi ya kuwa na mahusiano mazuri na watu pamoja na kutambua na kutumia fursa mbalimbali zinazojitokeza kwenye maisha yako.

kama ilivyo kwenye elimu ya msingi ya fedha jinsi inavyopatikana ndivyo ivyoivyo pia elimu ya Maendeleo Binafsi inavyopatikana.

tenga muda wako soma vitabu mbalimbali kuhusu Maeneo tofauti tofauti ya maisha, zungumza na watu waliofanikiwa katika kile unachotaka kufanikiwa, pia shiriki semina, makongamano na mikutano mbalimbali iliyo andaliwa kwa ajili ya kujifunza na utapata elimu hii muhimu.

Zungatia hata kama umekosa aina mbili za elimu zinazofundishwa shuleni. Ukiwa na aina izi mbili za elimu zisizofundishwa shuleni kwa dunia ya sasa Utafanikiwa Sana.

leo amua kuanza kuzitafuta elimu izi na utaona mabadiliko makubwa Sana kwenye maisha yako.

Mungu akubariki Sana kwa kujifunza.

weka katika matendo SoMo ili na utafanikiwa.

asante


Posted

in

by

Tags:

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *