Usiruhusu kushindwa kabla ujajaribu vya kutosha.

Katika maisha watu wengi sana wameshindwa kufikia mafanikio wanayoyataka siyo kwa sababu hawana uwezo wa kufanya ivyo, bali ni kwa sababu walikubali kushindwa kabla ya kuchukuahatua, na wengine walijaribu kidogo na kuitimisha kuwa haiwezekani.

hii inatokana na kuwa sisi binadamu ni viumbe tunaoongozwa na hisia na kabla ya kufanya maamuzi yoyote huwa tunakabiliwa na changamoto mbili kubwa ambazo ni hofu ya kushindwa na hofu ya kukataliwa.

Wengi wamekuwa wakishindwa kwa kujiambia mioyoni mwao kwamba nikifanya nitakosea, nikifanya nitashindwa nikijaribu nitakataliwa na wakati mwingine kusema haiwezekani kabla hata ya kujaribu.

ivi ni mara ngapi umetaka kufanya jambo fulani na kabla ya kufanya ukasikia sauti ndani yako ikikuzuia?

Ni mara ngapi ulitamani kumfuata mtu unayejua kuwa atakusaidia kutimiza ndoto yako lakini ukaogopa kuchukua hatua kwa kuamini kuwa atakukataa na kukwambia hapana.

najua hali hii imekukuta Sana na pengine ndiyo inayokusumbua na kukufanya usipige hatua maishani mwako

leo niko hapa kukwambia…..

… KAMWE USIKUBALI KUSHINDWA KABLA UJAJARIBU VYA KUTOSHA.

inawezekana kuna wakati ulijaribu na ukakataliwa mara kadhaa na ukusema basi nimejaribu vya kutosha lakini sijafanikiwa.

Mimi nakuambia bado unatakiwa ujaribu tena na tena na tena.

kuna wakati utakuta umeenda kwa mtu mara moja tu kuomba msaada flani lakini akakwambia hapana na ukavunjika moyo, Mimi nakwambia nenda tena kajaribu.

Haijarishi umekataliwa mara ngapi bado unaweza kukubaliwa, hapana ya mtu haimaanishi ndiyo itakuwa ivyo milele bado unayo nafasi ya kukubaliwa.

kuna watu huwa hawamkubali mtu mpaka awe amejaribu vya kutosha. Unapokataliwa haimaanishi kuwa una kasoro au udhaifu hapana watu wanakukataa kwa sababu zao wenyewe pengine kutoakana na mazingira au uitaji walionao wakati huo.

Na kwa wewe ambaye una ogopa kabisa kufanya jambo kwa kudhani kuwa watu watakukatalia au watakupinga, unapaswa kujua kwamba unajichelewesha mwenyewe watu hawana huo muda na Wala hata hawafikirii kufanya icho unachokiwaza.

Kitu cha muhimu hapo ni wewe kuchukua hatua ya kufanya na utaelewa kuwa yote uliyokuwa unaogopa hata hayapo ivyo.

ivi unajua kuwa asilimia Tisini na Tisa (99) ya mambo yote unayowaza na kufikiri kuwa yataenda ndivyo sivyo huwa hayatokei kama ulivyo fikiri?

unaweza ukawa shahidi wa ili pia

Mara ngapi ulikuwa na hofu ya kukataliwa na ukawa una ogopa kujaribu lakini ulipo thubutu kufanya wala hata ukukataliwa.

ni mara ngapi kwenye Kazi yako ulikuwa unaamini labda boss wako atakugombeza kwa makosa uliyofanya lakini hata haikuwa ivyo.

ni mara ngapi ulifikiri kwamba ukienda kwa mtu fulani kumweleza jambo lako atakukatalia na ulipo jaribu kwenda na kumweleza akakusaidia bila shida yoyote.

ni mara ngapi umeshindwa kwenda kuongea na wateja kwenye biashara yako kwa kufikiri kuwa watasema hapana na ulipo jaribu wote wakakubali na kununua bidhaa na Huduma zako.

hivyo ndivyo mambo yalivyo, Yale tunayoyahofia Sana ndani ya mioyo yetu huwa hayatokei kama tulivyo fikiri.

Hivyo acha kujichelewesha kwa kuogopa kuchukua hatua kisa tu watu watakukataa au utashindwa.

Chukua hatua bila uwoga, jaribu mara nyingi uwezavyo na kamwe usikubali kushindwa kuchukua hatua kwa sababu ya hofu uliyonayo ndani ya moyo wako.

Hofu na mawazo yote ya kushindwa uliyonayo ni kikwazo tu cha wewe kuto kuchukua hatua, na kama usipoipinga kwa kujilazimisha na kujisukuma kufanya utaishia kushindwa milele.

Dunia iko wazi na inaweza kukupa chochote unachotaka lakini yakupasa kuchukua hatua za kutosha ili kuthibitisha kuwa kweli una Nia ya dhati na unataka icho unacho kipambania.

kuanzia sasa usikubali kushindwa kabla ujajaribu vya kutosha kwenye kutafuta icho unachokitaka .

Naamini umejifunza sasa ni wakati wako, nenda kafanyie Kazi SoMo ili na utaweza kutimiza ndoto Zako na utapata chochote unachotaka kwenye maisha yako.

Mungu akusaidie Sana

Nenda kafanikiwe

asante


Posted

in

by

Tags:

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *