Ijue kanuni ya msingi Sana itakayokusaidia kupata pesa zaidi kwenye maisha yako.

Ndugu yangu mpendwa karibu kwenye SoMo letu zuri sana siku hii ya Leo tunapokwenda kujifunza kuhusu pesa.

kama ilivyo kawaida yetu tunaamka asubuhi na mapema tunaenda kupambana kuzisaka na kuzitafuta pesa.

Kuna msemo unasema Biashara asubuhi jioni ni mahesabu, ukimaanisha katika kila shughuri unayofanya kwenye maisha yako unatoa thamani Fulani ambayo ndiyo inakufanya ulipwe pesa. Na kwa kuwa ushazipata pesa sasa karibu kwenye mahesabu.

Wakati huu wa mahesabu naomba nikufundishe kanuni ya msingi Sana kuhusu pesa na kama utaielewa kanuni hii na kuanza kuifanyia Kazi sawasawa utafanikiwa Sana kifedha na utatimiza malengo yako ki rahisi zaidi.

kanuni yenyewe inasema

JILIPE MWENYEWE KWANZA:

hii ni kanuni nzuri Sana ya pesa ambayo umeishawahi kuisikia na kama bado, Leo kupitia Makala hii umepata bahati ya kuisikia na nataka uifanyie Kazi ili uone maajabu yake.

Kanuni ya jilipe mwenyewe kwanza inakutaka wewe ndugu yangu uchukue sehemu ya pesa yako uliyopata kwa siku, wiki, mwezi au mwaka kutoka kwenye shughuri zako za uzarishaji Mali na uitenge pembeni kwa ajili ya uwekezaji wako wa baadae.

kujilipa mwenyewe kwanza ni kuweka sehemu ya kipato chako pembeni na kutokukitumia kwenye matumizi yako na badala yake uwekeze zaidi.

katika hili unachagua kiasi Fulani cha kipato chako na kukiweka kwenye akaunti maalumu ambapo hauwezi kupafikia kirahisi.

Ili uweze kuiishi kanuni hii kwa mafanikio makubwa unapaswa kutenga sehemu ya kipato chako na kukiweka pembeni kabla hata ujaanza kuwaza kuhusu matumizi.

kanuni hii imejengwa kwenye msingi wa kuweka akiba na Kisha kutumia akiba hiyo kwa uwekezaji ili uweze kuzalisha zaidi.

Watu wengi sana kwa kukosa elimu ya msingi ya fedha pamoja na kutokuwa na nidhamu sahihi juu ya fedha wamekuwa wanaipuza kanuni hii kwa kuona kwamba hawana pesa ya kuwatosha kumudu maitaji Yao na ivyo hawataweza kutenga pembeni sehemu ya kipato chao.

Lakini pia kuna wengine ambao hawajui ni kiasi gani sahihi wanachotakiwa kujilipa wenyewe kwanza na kwa nini wanapaswa kujilipa wenyewe kwaza.

Sasa Makala hii itakupa majibu juu ya maswali hayo

kuhusu sababu ya kujilipa wewe mwenyewe kwanza ni kuweza kukusanya pesa kwa ajili ya uwekezaji utakaokusaidia katika maisha yako ya baadae.

ukiwa na pesa ni sawa na mkulima mwenye mbegu kama utaitumia pesa yako kuiwekeza kwenye maeneo ambayo yatakuzalishia pesa zaidi utanufaika kwa faida utakayopata sawa na mkulima ambaye amepanda mbegu zake kwenye shamba lenye rutuba anavyo furahia mavuno mengi.

kama ilivyo asili ya binadamu kadili tunavyoendelea kukua ndivyo nguvu zetu na uwezo wetu wa kufanya Kazi unazidi kupungua, nguvu ulizonazo Leo na uwezo wa kufanya Kazi ulionao Leo hautakuwa nao milele lakini matumizi yako na maitaji yako utaendelea kuwa nayo siku zote

ivyo mwenye busara ujiandaa kwa nyakati za baadae ambazo hataweza kuwa na nguvu za kufanya Kazi na kuingiza kipato na kile ulichojilipa mwenyewe kwanza na kuwekeza sehemu kwa ajili ya uzarishaji ndicho kitakacho kusaidia kwa nyakati za baadae.

Je ni kiasi gani sahihi cha wewe jujilipa mwenyewe?.

Ki msingi hakuna kiwango sahihi cha wewe jujilipa, kiasi chochote unachoona ni sahihi kulingana na kipato chako unaweza kuanza nacho, japo unashauliwa kuanza na angalau asilimia kumi ya kipato chako na kama autaweza anza na kiwango cha chini zaidi ya apo jambo la msingi ni wewe kujilipa na kutengeneza iyo tabia ndani yako.

Zungatia kiasi iki unachokiweka pembeni siyo kwa ajili ya dharura au matumizi yako ya baadae hapana. Pesa hii ni kwa ajili ya uwekezaji ili kuweza kuzalisha pesa zaidi na kukusaidia wewe kuwa na uhuru wa kipato.

Kama utaamua kuchukua hatua na kuanza kuifanyia Kazi kanuni hii nakuakikishia utaona mabadiliko makubwa Sana kwenye maisha yako na utaweza kujenga tabia ya msingi Sana itakayo kufikisha kwenye mafanikio makubwa Sana ya kifedha.

anza kuiishi kanuni hii sasa

Je kutokana na SoMo ili ni kiasi gani unaenda kutenga pembeni kwa ajili ya kujilipa mwenyewe kwanza ???

ikiwa utashindwa kuanza kuitumia kanuni hii na ukaitaji kujifunza zaidi kuhusu namna ya kujilipa mwenyewe kwanza unaweza kuwasiliana na Mimi kwa namba hii hapa

0754818580.

asante kwa kujifunza nenda kafanikiwe.


Posted

in

by

Tags:

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *