Kamwe usikate tamaa kwenye maisha yako.

Maisha ya mwanadamu yanafananishwa na safari ndefu Sana, safari ambayo inaanza siku unapozaliwa na itakamilika siku utakayoondoka hapa duniani.

katika safari hii kuna vipindi tofauti tofauti ambavyo lazima utavipitia na kuviishi. Kuna nyakati utakutana na mambo mazuri yenye kukufurahisha na kukupa furaha zaidi. Lakini kuna majira yatafika utakutana na mambo magumu, changamoto, tabu, shida na mateso mbalimbali ambayo yatakuumiza, kukudidimiza na kukukatisha tamaa kabisa kwenye maisha yako.

Mambo haya yote hufananishwa na milima na mabonde anayokutana nayo msafiri katika safari ya maisha yake na unapaswa kuwa tayari na kujiandaa sawasawa ili kukabili nyakati izi kwani kwa mtu yeyote aliye hai lazima atazipitia.

Kila mwanadamu huwa anapenda na kuzifurahia Sana nyakati nzuri zinazompa furaha katika maisha yake. Katika kipindi iki kila jambo huwa ni la kuvutia na kufurahisha.

Hapa utawaona watu wakifanikiwa katika mambo Yao mbalimbali kama vile kupata faida kwenye biashara, kupata Kazi, kutimiza malengo na ndoto zao, kupata familia nzuri, kuwa na afya njema, kupata mshahara, kupata watoto, kupandishwa cheo na mambo mengine mengi yanayoleta furaha na raha.

Yaani iki ni kipindi ambacho kila unachogusa kinageuka kuwa dhahabu.

Hakika nyakati izi ni nzuri Sana na kila mtu anae zipitia huwa ana hisia chanya juu ya maisha yake na ujiona mwenye thamani, mwenye uwezo mkubwa, mwenye Upendo na anapendwa na watu wengine, mwenye mafanikio na kila aina ya hisia nzuri.

Sasa jinsi maisha ya mwanadamu yalivyo yako kama shilingi yenye sura mbili,uwezi ukaishi siku zote za maisha yako kwa kuwa na uzoefu wa eneo moja tu na nyakati za aina Moja tu maishani.

Yaani uwezi kupitia maisha yenye furaha siku zote za maisha yako, uwezi kufanikiwa siku zote, uwezi kuwa na afya nzuri siku zote na uwezi kuwa juu ya wengine siku zote.

Kuna majira yatafika dunia itakulazimisha uujue upande wa pili wa shilingi , upande ambao umejaa shida, mateso na changamoto nyingi. Majira haya huwa yanatokea na ni sehemu ya msingi Sana katika maisha ya mwanadamu.

Majira haya yameumiza na kuangusha watu wengi sana kwenye maisha. Na kama wewe pia ni mmoja wa watu ambao umekuwa unateswa na nyakati ngumu basi somo ili linakuhusu wewe na mimi nipo hapa kukwambia kuwa……

KAMWE USIKATE TAMAA KATIKA MAISHA YAKO.

ni kweli utakutana na mateso, shida, changamoto na taabu mbalimbali katika maisha yako lakini kamwe usikate tamaa..

kuna wakati utafika kwenye maisha yako utapoteza kila kitu ulicho nacho sasa lakini usikate tamaa wala kuvunjika moyo.

kuna wakati utapoteza Kazi yako unayoitegemea, kuna majira utakataliwa na kuonewa kwenye Kazi yako lakini kamwe usikate tamaa.

kuna wakati utakutana na changamoto kwenye familia yako kama kupoteza wapendwa wako, kukosa mtoto, kukataliwa na mume au mke wako, ugomvi na kutokua na maelewano baina ya ndugu lakini kamwe usikate tamaa, endelea kusimama imara na kusonga mbele.

kwenye biashara yako. Kuna majira yatafika utashindwa kabisa kutengeneza faida, utakutana na ushindani na ugumu wa kila aina, biashara yako itakosa wateja, biashara yako itadumaa na kushindwa kukua, wateja watakuambia hapana lakini wewe usikate tamaa endelea kukomaa na biashara yako iyoiyo mpaka kieleweke.

unapaswa kujua kuwa kamwe nyakati ngumu huwa hazidumu milele ila watu wenye nguvu na wanao kataa kukata tamaa ndiyo huwa wanashinda na kudumu.

Kuwa na mtazamo chanya juu ya magumu unayopitia na kwa changamoto yoyote jua ni sehemu ya maisha tu na wala haitadumu milele bali inakupa uwezo wa kuwa imara na kuja kuwa mwenye mafanikio makubwa Sana pindi utakapo vuka.

Naamini kupitia somo ili utapata nguvu mpya ya kusonga mbele.

Sijui ni changamoto gani unayoipitia kwa sasa kwenye maisha yako, sijui ni kwa namna gani umeumizwa, sijui ni namna gani umeanguka lakini Leo nataka uamue kuinuka tena na kusonga mbele.

Wewe ni msindi na unastaili maisha yenye furaha.

Nenda kafanikiwe.

na Mungu akubariki na kukuongoza.

asante.


Posted

in

by

Tags:

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *