Unaona nini ndani yako.

Sisi wanadamu tumeumbwa katika namna mbili moja ni roho ( mtu wa ndani) na pili ni mwili ( mtu wa nje)

Namna tunavyoishi , jinsi tunavyofanya mambo mbalimbali na namna tunavyoenenda katika dunia hii inategemea Sana na kile kilicho ndani yetu.

akili yako ndiyo imeumba aina ya maisha unayoishi na ndiyo itakayoumba aina ya maisha utakayoishi. Ili limewezekana kupitia mawazo uliyonayo, maneno uliyosikia kutoka kwa watu wengine pamoja na Imani uliyonayo ndani yako lakini pia Imani uliyoipata kutokana na watu wengine kwa kusikia na kuona kwako.

kwa hiyo maisha yako hayatatoka nje ya kile ulichonacho ndani yako.

sasa ili kufikia mafanikio makubwa na kuweza kutimiza ndoto Zako kwa haraka Sana kuna jambo moja ambalo unatakiwa kufahamu kuhusu Akili yako na uanze kuitumia sawasawa.

kupitia ubongo wetu akili zetu sisi wanadamu huwa zinafanya Kazi Sana kwa kutumia lugha ya picha. Yaani unapokuwa na picha akilini mwako au unapoona picha fulani, ubongo wako unauwezo wa kuichakata, kuitafsiri, kuitunza na kuifanyia Kazi vizuri zaidi kuliko unavyofanyia Kazi maneno. Na ndiyo maana mtu anayejifunza kwa kutumia picha na michoro anauwezo wa kukumbuka vzuri zaidi kuliko yule anayejifunza kwa maneno ( maelezo).

Ivyo na wewe unatakiwa utumie nguvu hii ya ubongo kwa ajili ya kufanikisha malengo yako na kufikia mafanikio yako.

ndani yako, Yaani katika akili yako unatakiwa kuwa na picha kubwa juu ya ndoto zako, malengo uliyonayo, maisha unayotamani kuishi, afya unayotamani kuwa nayo, Mali na utajiri unaotamani kuumiliki pamoja na familia unayotaka kuwa nayo.

Kisha endelea kuicheza picha iyo kila siku kwenye akili yako. Kila siku itazame picha iyo kwenye akili yako. Fumba macho yako na tazama picha ya maisha yako iliyo akilini mwako kwa kutumia macho ya akili.naamini unaelewa ninaposema macho ya akili na kama uelewi jua tu kuwa akili yako inauwezo wa kuona kilicho ndani yako kama jinsi macho yako yanavyoona kile kilicho nje katika mazingira yanayo kuzunguka. Na unaweza kufanya zoezi moja kuthibitisha ninachosema, apo ulipo jaribu kufumba macho yako na utaona jinsi akili yako inavyoona picha zilizopo kwenye ubongo wako.

sasa unapokuwa na picha kubwa ya vile unataka kuwa pamoja na kwa yale unataka kutimiza maishani mwako. Unaifanya akili yako itumie uwezo wake pamoja na kutumia uwezo wa dunia ( nguvu ya dunia ) kuvuta na kutengeneza mazingira yayakayokusaidia kufikia mafanikio ya icho unachokiona.

na katika ili naomba nikuongezee kitu kimoja kitakacho chochea mafanikio yako kwa haraka zaidi. Unapokuwa unaicheza na kuitazama picha ya maisha yako akikisha unaiona kama ni kitu halisi ambacho tayari kimeshatokea. Katika hili anza kujiona tayari unaishi katika nyumba ya ndoto yako, anza kuona unavyotumia utajiri ulioutengeneza, anza kujiona kama tayari uko katika nafasi ya uongozi unayotamani na anza kuona kama tayari unakiliki biashara yako.

Tafiti zinaonyesha kuwa ubongo wetu unaudhaifu wa kushindwa kutofautisha kitu halisi na kitu ambacho ni picha hasa picha ivyokuwa inarudiwa rudiwa kuchezwa ndani ya akili.

kupitia udhaifu huu ubongo wako una amini picha Ile kama kitu halisi na utakusaidia kutengeneza mazingira na kukupa fursa ya wewe kuweza kufanya jambo litakalo kuwezekana kufikia maono yako kama yalivyo kwenye picha unayoiona.

hii ni Siri ambayo watu waliofanikiwa wameweza kuitumia na ikawasaidia kufanikisha malengo na ndoto zao hata wewe unaweza kuitumia kwani bado inafanya Kazi sawasawa na ni Siri ambayo wengi hawaifahamu.

kuanzia leo akikisha unakuwa na picha kubwa ya jinsi unavyotaka kuwa kwenye maisha yako na kila siku usiku kabla ya kulala na asubuhi baada ya kuamka akikisha unaicheza picha iyo akilini mwako

kadili unavyoendelea kucheza picha ya maisha yako ndivyo utakavyo vutia fursa na njia mbalimbali ambazo ukizitumia sawasawa utaweza kutimiza ndoto Zako

Je wewe unapicha ya kile unataka kwenye maisha yako??

je akilini mwako unaona nini juu ya maisha yako..?

endelea kufatilia ukurasa huu kwa masomo zaidi.

pia kama unataka nikusaidie katika kutimiza ndoto yako wasiliana nami kwa namba

0754818580.

asante .


Posted

in

by

Tags:

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *