kuwa tayari kuanzia chini.

Mtu yeyote mwenye ndoto kubwa maishani lazima awe tayari kuanza kuishi ndoto yake kwa kufanya mambo mbalimbali ili kuipa uhai ndoto iyo . Na msingi mzuri hapa ni kujua kuwa atatakiwa kuanzia chini kabisa.

watu wengi sana wamekufa na ndoto zao na wengine wanaendelea kuishi bila kutimiza ndoto zao kwa sababu wanaona kama bado hawana kila kitu wanachoitaji ili kuanza kufanya utekelezaji. Hii inatokana na kuwa wengi wanatamani kuanza na kutekeleza kwa ukubwa wa picha walionayo akilini.

wanatamani wanapoanza tu wawe na mafanikio makubwa wanayoyatamani, wengine wanatamani wakianza wawe kama watangulizi wao kwenye kitu icho wanachofanya.

Jambo ili limekuwa ni kikwazo kikubwa Sana cha ndoto nyingi kufa.

Ili uweze kufanikiwa katika maisha na kutimiza ndoto yako lazima ukubali kuanzia chini kabisa, kubali kuwa na mwanzo mdogo unaokupeleka kwenye ndoto yako kubwa.

hakuna hata mtu mmoja aliyefanikiwa kwa kuanzia juu, watu wote waliofanikiwa walianzia chini. tena kuna wengine wamefanikiwa lakini mwanzo wao ulikuwa mbaya Sana na wengine walianza wakiwa katika hali mbaya zaidi kuliko hata hali uliyonayo wewe lakini walikubali na kuamua kufuata mchakato na mwisho wa siku wakafika juu.

chochote kile kinaanza na moja. Kuelekea kwenye elfu 1000.

ukianzisha kufanya biashara utaanza na mteja mmoja na utaendelea kwa hatua izo mpaka kufikia kuuza kwa wateja 1000

ukianza kuandika kitabu utaanza na neno moja Kisha ukurasa mmoja mwisho wa siku utafika kuwa na kitabu chenye kurasa 1000

Hata katika maisha mtu unazaliwa na kuanza kuiishi siku mojamoja ukiwa hauna kitu na unaendelea ivyo mpaka unafikia kufanikiwa

Hata ghorofa lilianza kwa kujengwa tofali mojamoja mwisho wa siku likakamilika

Kuna msemo unasema safari ya maili elfu moja (1000) inaanza na hatua moja.

usiruhusu ndoto yako kufa ndani yako kwa sababu tu ujawa tayari. Anza kuiishi ndoto yako sasa, amua kuanzia chini kabisa na kufuata hatua ndogo ndogo na mwisho wa siku utafanikiwa…

Naamini utakwenda kuanza kuishi ndoto yako na hauta dharau mwanzo mdogo

endelea kujifunza kila siku kupitia blog hii na maisha yako yatabadilika.

leo kama utatamani nikusaidie kutimiza ndoto yako wasiliana nami kwa namba 0754818580 nami nitakusaidia

asante


Posted

in

by

Tags:

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *