Ndoto Yako Inawezekana.

Ndugu yangu mpendwa karibu sana kwenye blog hii ya Timiza Ndoto Academy sehemu ambayo unakwenda kujifunza na kubadilisha maisha yako kabisa kupitia makala mbalimbali katika maeneo ya Maendeleo Binafsi, elimu ya msingi ya fedha, elimu ya msingi ya biashara na maisha kwa ujumla.

Ndugu yangu kila mmoja wetu ana ndoto kubwa ambayo inaishi ndani yake. Kila mmoja wetu ana kusudi na sababu ya yeye kuumbwa na kuwepo hapa duniani. Lakini umekuwa unashindwa kujua ufanye nini ili kutimiza ndoto hiyo.

sasa hapa ni mahali sahihi Sana kwa wewe kujifunza na kupata maarifa sahihi yatakayo kusaidia kuchukua hatua na kufikia ndoto yako.

Ndoto uliyonayo inawezekana haijalishi uko katika hali gani, haijarishi uko katika mazingira gani ila leo nakuambia kuwa ndoto yako ambayo umekuwa nayo ndani ya moyo wako kwa muda mrefu inawezekana kabisa kuifikia.

sasa kwa yeyote mwenye ndoto kubwa kuna mambo Saba (7) ambayo anatakiwa kuyazingatia ili kufikia ndoto iyo.

1. IMANI THABITI. JUU YA NDOTO YAKO

jambo la kwanza na la muhimu kabisa kuwa nalo ni Imani. Hapa ndipo ndoto yako inaanzia kujengwa. Unapokuwa na Imani sahihi juu ya ndoto yako unatengeneza mazingira mazuri Sana kwa wewe kuifanikisha.siku zote unapaswa kuwa na mtazamo chanya kuhusu icho ulichonacho, amini kuwa unaweza kufanya na ukafanikiwa, amini kuwa wewe ndiyo mtu sahihi wa kufanya, amini kwamba kila kitu kinawezekana. Hata siku Moja usiruhusu mawazo hasi, hata siku Moja usiamini katika kushindwa licha ya kuwa kuna wakati utakutana na mawazo ya kushindwa lakini kataa mawazo hayo na endelea kujaza akili yako kwa mawazo ya uwezekano.

Kupitia mawazo unaumba hatima ya ndoto yako. Ukiamini katika uwezekano utavutia fursa na mazingira yote ya kufanikiwa kuja kwako na utatumia mazingira hayo kufanikisha

Lakini ukiamini katika kushindwa utavutia vikwanzo, vizingiti, kughairisha na kukata tamaa na mwisho wa siku hautafanikiwa.

Ivyo anza kwa kuwa na mawazo chanya juu ya ndoto yako ili ujiweke katika mazingira mazuri ya kufanikiwa katika icho unachotamani kuwa.

2. KUWA NA MAONO MAKUBWA

jambo la pili la kufanya ili kutimiza ndoto yako ni kuwa na maono makubwa.

Anza kujiona katika nafasi unayotamani kuwa, anza kuona mafanikio yako katika eneo la ndoto yako. Kuwa na picha ya ndoto yako kichwani na endelea kuitazama kwa kutumia macho ya akili yako.

jambo unalotakiwa kulijua ni kuwa unapokuwa na maono makubwa na picha kubwa ndani yako ya kule unakotaka kufika, akili yako itakusaidia kukutengenezea mazingira ya wewe kufika.

ubongo wako una kasoro ya kutofautisha vitu, yaani hauwezi kutofautisha kitu halisi na kitu ambacho siyo halisi hasa pale kinapo kuwa kinaonekana mara kwa mara

kwa mfano wewe unapokuwa na picha kubwa ya ndoto yako akilini labda unajiona kuwa ni mtu mkubwa uliyefanikiwa, au unajiona umeweza kutimiza ndoto yako kubwa uliyonayo kama kumiliki biashara, kuwa mzungumzaji mkubwa, kuwa mwandishi nguri wa vitabu, kuwa na familia nzuri, kuwa na afya nzuri, kushinda kwenye mashindano katikamichezo au kupata Kazi ya ndoto yako.

ukiendelea kuona picha iyo kila siku ndani ya akili yako mwisho wa siku utatengeneza mazingira na njia ya kufikia ndoto iyo. Jambo hili ni la uhakika kabisa na limesaidia watu wengi sana kufikia ndoto zao

ivyo kuwa na picha kubwa ya kule unakotaka kufika na utaweza kufika.

3.WEKA MALENGO

Jambo la tatu la kuzingatia kwa anayetaka kutimiza ndoto yake ni kuwa na malengo

malengo ndiyo yatakusaidia wewe kuwa na dira na utajua unatakiwa kufanya nini, wakati gani na kwa nini ufanye. Hivyo unatakiwa kukaaa chini na kupanga malengo yako

Hapa unapanga malengo ya muda mrefu, muda wa Kati na Muda mfupi kuhusu ndoto yako na unaakikisha malengo uliyoyaweka yanaendana na ndoto yako. Katika hili lazima upange malengo ambayo ni mahususi yenye kutekelezeka, kupimika na yaliyo fungwa kwenye muda. Kisha kuwa na vipaumbele vya utekelezaji wa malengo hayo

Kumbuka ni kupitia kuweka malengo ndiyo utapata msukumo wa kuchukua hatua kuelekea ndoto yako na malengo utakayo panga hayatakiwi kuwa kichwani tu bali lazima yawe katika maandishi kwenye karatasi.

4. KUWA NA UTHUBUTU.

jambo la nne na la msingi Sana kwa mtu mwenye ndoto kubwa ni kuamua kuingia moja kwa moja kwenye utekelezaji wa ndoto iyo. Hata siku Moja usije ukategemea kuwa ndoto uliyonayo itatimia kwa fikra peke yake au kwa kuwa na mtazamo chanya na kwa kuwa na picha kubwa ndani yako hapana

ndoto yako kuweza kutumia inakuitaji wewe kuthubutu, unaitaji kuingia katika kuifanyia Kazi ndoto yako. Kuthubutu ni kuamua kuanza kuiishi ndoto yako bila kujali uko katika hali gani.

unaitaji kuanza kuchukua hatua bila kuangalia mazingira, Wala kusubiri kila kitu kuwa sawa unatakiwa kuanzia hapohapo ulipo kwa ichoicho ulichonacho mkononi mwako

mwenye uthubutu atumii muda mwingi kufikiri namna ya kuanza yeye anaanza na kuendelea kuboresha kidogo kidogo kadiri siku zinavyoenda.

Kuwa na ndoto bila kuchukua hatua hakuwezi kukufanikisha na kukufikisha kwenye mafanikio. Lakini uthubutu ndiyo utakaokufikisha pale unapotaka

anza sasa kuweka ndoto yako kwenye matendo na utafanikiwa.

5. FANYA KAZI KWA BIDII.

Jambo la Tano kwa mtu anayetaka kutimiza ndoto zake ni kufanya Kazi kwa bidii. Msingi wa mafanikio uko kwenye kazi, ni kupitia kufanya Kazi ndiyo utaweza kufanikiwa, ivyo kama una ndoto kubwa punguza maneno ya mdomo na ongea kwa vitendo zaidi.

kumbuka kuwa vitendo vina sauti na vinasikika na kuonekana zaidi kuliko maneno. Kila siku akikisha unafanya jambo kwa ajili ya ndoto yako. Fanya kitu hata kama ni kidogo lakini akikisha kinaongeza kitu kwenye kufikia ndoto yako

kupitia kujituma na kufanya Kazi kwa bidii lazima utafanikiwa tu kwani juhudi hazidanganyi na hazijawai kumsaliti mtu yeyote ambaye ameweka Kazi kwa bidii.

6. JIFUNZE KILA SIKU

Jambo la sita la msingi kwa mtu mwenye ndoto kubwa ni kuendelea kujifunza kila siku . Ndugu yangu Leo upo hapo ulipo kwa sababu ya maarifa na taarifa ulizonazo. Yaani elimu na mambo Yale unayoyajua ndiyo yamekufikisha hapo ulipo. ivyo ili kuweza kutoka apo na kufika katika ndoto yako unatakiwa ujifunze na kufahamu mambo mapya.

Dunia tunayoishi inabadilika kila siku ivyo usipojifunza utaachwa nyuma. Kile ulichokuwa unakijua Jana Leo kinaweza kisifanye Kazi na ukweli wa Jana Leo unaweza kuwa ni uongo ivyo kuendelea kujifunza kila siku ndiyo msingi wa wewe kupata ujuzi mpya na utaweza kupiga hatua kwa Kasi Sana

kubali kuonekana mjinga ili ujifunze, acha kuamini kuwa unajua kila kitu, kuwa mpole na tafuta maarifa kila siku. Watu wote waliofanikiwa na kutimiza ndoto zao ni watu wanaojifunza kila siku. ivyo ili na wewe uweze kufanikiwa lazima uwe mwanafunzi maisha yako yote.

hapa siyo kwamba lazima urudi shule kujifunza kwa mfumo rasmi hapana dunia tuliyonayo sasa inakuwezesha kujifunza ukiwa mahali popote pale. Soma vitabu, uzulia semina na kozi mbalimbali, tumia simu yako kusoma, fatilia video za mafunzo kwenye mtandao, soma makala kwenye mtandao kila maarifa unavyoitaji kutimiza ndoto yako unayo kwenye mkono wako dunia ni Kijiji, jifunze bila kukoma.

7. KAMWE USIKATE TAMA.

Jambo la Saba la kuzingatia ili kutimiza ndoto yako ni kutokukata tamaa. Ndugu yangu ni kweli safari ya wewe kuelekea kwenye ndoto yako haiwezi kuwa rahisi kama unavyofikiria, lazima kuna mapito ambayo utapitia. ivyo kuwa tayari kupita kwenye mapito hayo bila kukata tamaa.

utakapoanza kuishi ndoto yako, utakapoanza kujituma kwa ajili ya ndoto yako utapata upimzani mkubwa Sana. Kuna wakati utakataliwa , kuna majira yatafika utapingwa tena na watu wa karibu yako, kuna wakati utatengwa, kuna wakati utaanguka, kuna wakati utapata hasara na kupoteza rasilimali zako lakini kuwa tayari kuvumilia maumivu yote na kamwe usikate tamaa

watu waliotiza ndoto zao ni watu wenye mioyo migumu Sana. Ni watu ambao walikubali kuteseka na kuumia walipo pitia nyakati ngumu lakini hawakukubali kukata tamaa na ndiyo maana wamefanikiwa.

ivyo kuwa tayari kupitia mateso yaliyo na mwisho ili utimize ndoto yako. zingatia Sana ili kwamba haijalishi utapitia katika hali gani kamwe usikate tamaa.

Ndugu yangu kuanzia Leo anza kuamini kuwa ndoto yako inawezekana na chukua hatua kwa kuzingatia mambo haya Saba niliyokuandikia na utafanikiwa Sana.

asante kwa kuwa umejifunza

Kwa msaada zaidi kuhusu namna ya wewe kutimiza ndoto Zako wasiliana na mimi moja kwa moja kwa mawasiliano yaliyo chini ya makala hii na nitakupa muongozo mzuri kabisa .

0754818580

mwl.Baraka Paulo