Ukiwekeza kwenye iki basi utafanikiwa Sana

Toka enzi na enzi watu wamekuwa wakitafuta mafanikio kupitia shughuri mbalimbali.

Kuna ambao wamekuwa wakifanya Kazi za kuajiriwa na wengine kujikita katika shughuri zao binafsi ikiwemo biashara, kilimo pamoja na ufugaji kwa lengo la kutafuta mafanikio na kuwa na furaha maishani.

Lakini watu wengine ikiwemo wale walioweza kufikia mafanikio ya juu zaidi wamekuwa wakisema wao waliweza kufikia uko kupitia uwekezaji

kuna ambao wamewekeza kwenye biashara kubwa, wengine ni uwekezaji katika majengo, uwekezaji katika mashamba makubwa na mazao ya muda mrefu, uwekezaji katika hisa, uwekezaji katika dhamana za serikali, uwekezaji katika Mifuko ya pamoja, uwekezaji kwenye mabenki na kwa dunia ya Leo kuna uwekezaji katika sarafu za mtandao yaani cripto currency.

Yote hayo pamoja na mengine mengi ambayo sijayataja hapo ni Maeneo mbalimbali ambayo unaweza kuwekeza na ukapata mafanikio makubwa Sana. lakini bado siyo uwekezaji ambao tunaweza kusema ni wa kweli na wenye kukufaa kwa maisha yako yote.

Sasa kabla ujaamua ni kwa namna gani unataka kufanya uwekezaji, Leo nina kufundisha moja ya uwekezaji ambao una faida kupita uwekezaji wa aina nyingine yoyote. Na aina hii ya uwekezaji ni ule UWEKEZAJI UNAOUFANYA NDANI YAKO WEWE MWENYEWE:

Ndugu yangu mpendwa kama kweli unataka kufanikiwa na kufika mbali maishani basi kitu cha kwanza lazima uangalie kuhusu kuwekeza ndani yako.

Ndani yako kuna vipawa, karama, na uwezo mkubwa Sana ambao kama hautaweza kuviibua utaishi maisha yako yote bila kuvitumia,

Yakupasa ufahamu kuwa kwenye maisha kabla ya wewe kufikia mafanikio makubwa yanayoonekana kwanza unatakiwa ufikie mafanikio makubwa ndani yako. Kile unachotaka kukionyesha kwa nje katika ulimwengu huu kinatakiwa kwanza kiwe kimeonekana ndani yako.

Ukubwa na urefu wa ghorofa linaloonekana na kusifiwa na watu umeshikiliwa na msingi mkubwa imara na mrefu kwenda chini ambao hauonekani. Hivyo basi chochote kikubwa na chenye mafanikio nyuma yake kuna Siri kubwa Sana ambayo haionekani

Hivi ndivyo ilivyo hata kwako na ndiyo maana nasisitiza kuhusu kuwekeza ndani yako ili ufanikiwe zaidi.

Sasa kwa nini kuwekeza ndani yako ndiyo uwekezaji wenye thamani kubwa na faida kubwa kuliko aina nyingine yoyote ya uwekezaji?.

Moja UTAKUWEZESHA KUKUA ZAIDI. Unaitaji chakula ili uweze kukua, chakula cha mwili kitakupa afya njema, chakula cha kiroho kitakupa afya njema ya kiroho lakini chakula cha kiakili kitakusaidia kuweza kupanuka na kuwa mwenye mawazo mapana Sana na kuona mambo kwa utofauti mkubwa.

Ili linawezekana kwa kuwekeza ndani yako kupitia kujifunza zaidi hasa kwa kusoma vitabu, kufatilia mafunzo mbalimbali kupitia semina, makongamano, ushauri kwa waliofanikiwa, kusoma Makala na kuangalia video zenye mafunzo ya kujenga.

Mbili. UTAEPUSHA KUFANYA MAKOSA MENGI:

Safari yoyote ya kutafuta mafanikio imejaa milima, mabonde na changamoto nyingi. Mchakato wa mafanikio unahusisha kukosea mara nyingi na kuchukua hatari mara nyingi ambapo kama hautakuwa na msingi sawasawa utajikuta unapoteza kila siku. Sasa kupitia uwekezaji ndani yako utaweza kujifunza na kupata uzoefu wa watu mbalimbali waliokutangulia kwenye mafanikio na utaweza kuepuka makosa mbalimbali ambayo wao waliyafanya kwenye maisha na kupitia wao wewe hayatakukuta.

Tatu: UTAONGEZA UZARISHAJI KWA UFANISI MKUBWA

Misingi imara ya maarifa na ujuzi utakaokuwa umeujenga ndani yako kupitia uwekezaji utaweza kufanya majukumu yako kwa ubora na ufanisi wa hali ya juu na mwisho wa siku uzarishaji wako utakuwa wenye manufaa na faida kubwa.

Nne: UTAONGEZA UWEZO WAKO WA KUJIAMINI:

Wakati mwingine watu wameshindwa kufanikiwa kupata kile wanachokutafuta kwa sababu tu waliokosa kujiamini kupitia uwekezaji ndani yako utaweza kuwa na ufahamu wa mambo mbalimbali jambo ambalo litakupa kujiamini Sana.

Tano: UTAWEZA KUTAMBUA THAMANI YA MAISHA:

kwenye maisha uwezi kujua thamani yako na thamani ya maisha uliyonayo kama bado ujajua kusudi la kuumbwa kwako na nini yakupasa ufanye ili kuliishi na kulitimiza kusudi hilo. Kupitia kuwekeza ndani yako unaweza kutambua yote hayo kwani utapata nafasi ya kudadisi kile kilicho moyoni mwako kwa ukaribu zaidi kupitia misingi ya tahajudi utakayo kuwa umejifunza.

Sita: UTAWEZA KUTAMBUA VIPAJI NA UWEZO MKUBWA ULIOLALA NDANI YAKO:

Moja ya sehemu kubwa yenye utajiri hapa duniani inasemwa kuwa ni makaburini, kwani kuna watu wengi wenye vipaji na uwezo mkubwa ambao ungeweza kubadirisha kabisa maisha yao lakini hawakuutumia, hii inatokana kuwa walishindwa kuutambua uwezo huo kama uko ndani yao au wakati mwingine waliokosa kujiamini na kushindwa kuitumia.

Lakini kwako wewe kupitia kuwekeza ndani yako utapata nafasi ya kujua vipawa na uwezo mkubwa ulio nao na utaweza kuutumia na kuwa na mafanikio makubwa.

Saba: UTAJUA NAMNA BORA YA KUJENGA MAHUSIANO;

Dunia tuliyonayo ni dunia ya kuhusiana na yeyote atakayekuwa na ujuzi na uwezo wa kuhusiana na watu ndiyo atakayekuwa na mafanikio makubwa. Kwani kila kitu unachoitaji ili kufanikiwa utakipata kwa mtuwingine, Sayansi na Sanaa ya kujenga mahusiano utaipata na kujifunza kupitia uwekezaji ndani yako.

Nane: UTAWEZA KUONA FURSA KABLA YA WENGINE NA KUJIONGEZEA BAHATI KWENYE MAISHA YAKO

Siku zote tunasema mafanikio utokea pale ambapo maandalizi yanakutana na fursa. Sasa kupitia uwekezaji ndani yako ndiyo maandalizi yenyewe na kupitia maandalizi hayo utaweza kuzitambua fursa mbalimbali zinazojitokeza mbele yako na kwa kuwa una msingi imara utaweza kujua fursa nzuri na utazitumia kufanikiwa.

Tisa UIMARA KIHISIA

Moja ya jambo kubwa ambalo limewakwamisha watu wengi kufanikiwa ni namna ya kutawala hisia zao.

Ukweli ni kuwa sisi binadamu ni viumbe wa kihisia na tumekuwa watu wa kufanya maamuzi mengi Sana kwa kutumia hisia na siyo akili. hivyo kama ujaimalika sawasawa katika swala la kihisia lazima uta kwama mahali,kwa kushindwa kufanya maamuzi mazuri. na ni kupitia uwekezaji ndani yako ndiyo unaweza kukusaidia kuwa imara kihisia.

Kumi: HUTAKUWA MTU WA MALALAMIKO:

Watu wengi wanapokutana na changamoto kwenye maisha yako cha kwanza huwa wanatafuta ni nani kasababisha ili waweze kumlaumu. Hapa utakuta watu wakilaumu serikali, wazazi, walimu, marafiki na makundi mengine ya watu kwa kuamini kuwa kile wanachokipitia kwenye maisha kimesababishwa na watu hao, bila kujua kuwa chochote kinachotokea maishani kimesababishwa na wewe mwenyewe.

kupitia uwekezaji ndani yako utaweza kujua ukweli na utaona kuwa wewe ndiyo unawajibika na maisha yako kwa asilimia mia moja na kama kuna mahali umeshindwa ni kwa sababu yako wewe mwenyewe.

Ndugu yangu mpendwa faida za wewe kuwekeza ndani yako zipo nyingi Sana naweza kuadika na nisizimalize lakini naamini mpaka hapo nilipofika utakuwa umepata maarifa ya kutosha na umeona jinsi uwekezaji huu ulivyo na thamani kubwa kwako.

Naomba kuanzia Leo kabla ujafanya jambo lolote kwenye maisha iwe ni Kazi, biashara au uwekezaji kwanza anza kujenga msingi kwa kuwekeza ndani yako. Kwa kufanya ivyo utafanikiwa Sana

Mungu akubariki Sana kwa kuweza kujifunza, nenda kaweke kwenye matendo SoMo ili hili uweze kufanikiwa na kuwa na maisha yenye maana.

Nenda kafanikiwe.


Posted

in

by

Tags:

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *