Ushindi unatengenezwa

kila mtu aliyepo hapa duniani amezaliwa akiwa na uwezo wa kipekee Sana ndani yake.

Kila mmoja alipewa vipaji, karama na mambo mengine mengi mazuri ambayo kama akiyatumia vizuri anaweza kufanikiwa na kuwa na maisha yenye kugusa watu wengi na kuacha alama kwa kuifanya dunia kuwa sehemu bora zaidi ya kuishi kutokana na maajbu atakayo kuwa ameyafanya.

lakini sasa licha ya kuwa na uwezo mkubwa ndani yetu bado dunia imefanya Kazi kubwa Sana na kuiba kile kilichowekwa kwa kutudanganya na kituaminisha kuwa siyo kila mmoja anauwezo wa kufanikiwa na kuwa mshindi kwenye maisha.

Hili limewezekana kwa kupitia mafundisho mbalimbali kutoka kwa watangulizi wetu ikiwa ni pamoja ya wazazi wetu, walimu wetu na jamii ya watu wanao kuzunguka ambao kwa pamoja wamekufundisha mambo mengi ambayo kwa namna moja ama nyingine ndiyo yamechangia wewe kuwa apo ulipo Leo.

Kutokana na ilo watu wachache ndiyo wameweza kufanikiwa uku kundi kubwa likibaki kuwa na maisha ya kawaida na wengine wakiwa hawaelewi hata hatima yao.

Hivyo basi kwa kuwa wewe ni mshindi tayari na umezaliwa ili kushinda,……….,

Leo kuna jambo moja ninataka nikueleze ili likusaidie kubadilisha maisha yako.

Iko ivi mpendwa kwa kuwa umezaliwa ili kushinda lazima utambue kuwa

USHINDI UNATENGENEZWA

Na ili uweze kushinda na kuwa na mafanikio lazima ukubali kufuata mchakato na kuzingatia mambo haya matatu ambayo ni kuwa na mpango wa kushinda, kujiandaa kushinda na mwisho kutegemea kushinda.

Sasa ebu tuangalie kwa kina mambo haya matatu.

Jambo la kwanza: PANGA KUSHINDA.

Katika hili kila mtu anayetaka kufanikiwa na kupiga hatua kubwa maishani lazima kwanza ajue msingi muhimu Sana wa kufanikiwa ambao ni kuwa na Maono makubwa ya nini hasa anataka kwenye maisha yake

Kisha unafata kwa kuweka Malengo mahususi pamoja na mikakati ya namna gani utakwenda kufanya ili kufikia mafanikio yako yatakayo kuletea ushindi kwenye maisha.

Kwa kuzingatia mambo hayo juu ya kupanga malengo na kusimamia maono uliyonayo uwe na uhakika kabisa lazima ufanikiwe,

Jambo la pili ni KUJIANDA KUSHINDA

Ili liko wazi kabisa kuwa yeye anayekubali kuvuja jasho jingi wakati wa mazoezi ndiye atakaye vuja damu kidogo Sana wakati wa vita.

Na yeyote atakayejiandaa vizuri kwa habari ya kutafuta mafanikio hata wakati ambapo haoni njia ndiye atakaye kuwa na mafanikio makubwa Sana pale njia inapopatikana.

Na hii ndiyo maana huwa hakuna bahati kwenye maisha ya kutafuta mafanikio Bali mafanikio huwa ni matokeo ya maandalizi yakikutana na fursa.

Hivyo basi kwa yeyote anayetaka kufikia ushindi ambao tayari amezaliwa nao yampasa kutambua umuhimu wa kuwa na maandalizi.

lazima ujiandae kwa kuakikisha kila kitu unachoitaji ili kufanikiwa unakuwa nacho.lazima ujiandae kuanzia fikra zako, akili yako, Imani yako, elimu inayotakiwa, ujuzi unaotakiwa pamoja na ushauri utakaoitaji kutoka kwa watu wengine ambao wamekutangulia katika kile unataka kufanikiwa .

Jambo la tatu ni KUTEGEMEA KUSHINDA.

Mafanikio siku zote yako wazi na yanafata kanuni ambazo ni za kweli.

Kuna msemo unasema kama njia iliyotumika ni sahihi basi na majibu nayo yatakuwa ni sahihi pia.

Kama kweli ulikaa chini ukapanga kufanikiwa kwa kuwa na Maono pamoja na kuweka malengo na namna ya kuyafanikisha,. alafu ukajiandaa vya kutosha kwa kufanyia Kazi Yale yote yaliyopaswa kufanyika. Basi swala la mafanikio kwako linakuwa ni rahisi Sana.

Kwa kuzingatia mambo yote hayo kumbe sasa kwenye hatua hii ya kutegemea kushinda ndipo tunapata uhakika wa mafanikio na kufikia ushindi wetu.

Ivyo ndivyo ilivyo…

Naamini umejifunza kitu na utaenda kuweka kwenye matendo ili ufanikiwe

kwa namna yoyote ukiitaji usimamizi na ushauri wa jinsi gani unaweza kufanya na kufikia ushindi wako wasiliana nami kwa namba 0754818580

Na Mimi nitakusaidia.

Mungu akusaidie Sana katika utekelezaji wa somo ili

Nenda kafanikiwe kutengeneza ushindi kwenye maisha yako.


Posted

in

by

Tags:

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *