Sababu kuu tatu kwa nini waajiriwa wengi wameshindwa kuanzisha biashara nje ya ajira

Watu wengi sana ambao wameajiriwa wamekuwa na changamoto moja kubwa Sana inayo wakabili katika maisha yao ambayo ni kushindwa kufikia uhuru wa kipato.

Jambo ili limechangiwa zaidi na wao kutegemea chanzo kimoja cha kipato hali inayowafanya washindwe kupiga hatua kubwa maishani, kwani licha ya kuwa wengi wao wana pambana kufanya Kazi kwa bidii bado sehemu kubwa ya kipato chao inamezwa na matumizi walio nayo.

Na kwa kua changamoto hii imezidi kuwa kubwa kwa wengi, Elimu imekuwa ikitolewa kuwashauri waajiriwa kufikiri ni namna gani wanaweza kuanzisha biashara za pembeni nje ya ajira zao wanazozifany.

kwa sababu kupitia biashara kuna uwezekano mkubwa wa kutengeneza kipato kikubwa na kupiga hatua kubwa Sana kwenye maisha kuliko ilivyo kwenye ajira.

Hili linatokana na kuwa ajira zina ukomo wa kipato na biashara hazina ukomo wa kipato, kadiri utakavyo weka juhudi na jitihada kufanya biashara yako kwa bidii na kufikia wateja wengi zaidi ndipo utakapo furahia matokeo yake na kupata pesa zaidi.

Sasa licha ya kuwa ushauri wa kuanza biashara nje ya ajira umekuwa ndiyo ushauri mzuri na wenye kuleta matumaini kwa waajiriwa, bado waajiriwa wengi wameshindwa kuufanyia Kazi sawasawa kwa sababu kuu tatu ambazo ndiyo tunakwenda kuziangalia hapa chini.

Sababu ya kwanza ni : KUKOSA WAZO LA BIASHARA

Hii ni Moja ya sababu kubwa Sana inayowaumiza waajiriwa wengi na kuwafanya washindwe kuanzisha biashara nje ya ajira zao.

wengi wao wanaamini kuwa biashara ni mkombozi kwao lakini hawajui wafanye biashara gani, hawajui namna ya kupata wazo bora la biashara, na wamekuwa wanaamini ili kuweza kuwa mfanya biashara mwenye mafanikio makubwa basi kuna biashara za aina fulani wakizifanya basi watafanikiwa Sana.

Ukweli ni kwamba ili kuweza kupata wazo bora la biashara kwako wewe uliyeajiriwa yakupasa uzingatie mambo haya mawili

Jambo la kwanza ni matatizo gani ambayo watu wanapitia na wewe unaweza kuyatatua na wakakulipa pesa au ni maitaji gani watu wanaitaji na wewe unaweza kuwasaidia kuyapata na wao wakakulipa pesa.

Na ili kujua matatizo na maitaji ya watu anza kwanza na yale yanayo kukabili wewe mwenyewe Kisha angalia kwenye jamii yako, kwa kufanya ivi utaweza kupata wazo bora la biashara na watu watakua tayari kukulipa kwa thamani uliyotengeneza.

jambo la pili la kuzingatia katika kupata wazo bora la biashara ni kupitia vitu unavyovipenda.

Kaa chini na angalia Yale unayopenda Sana kufatilia na kuyafanya alafu yageuze kuwa biashara yako. Mfano kama unapenda Sana nguo angalia namna ya kuuza nguo, kama unapenda Sana kupika basi geuza mapishi yako kuwa biashara kwa kupika moja kwa moja au kufungua biashara inayohusiana na mapishi kama vile kufundisha watu mapishi au kuuza vyombo.

Kwa kufanya ivyo utakuwa umejipatia wazo la biashara.

Zingatia hakuna aina fulani ya biashara ambayo imethibitishwa kwamba kama kila mtu ataifanya iyo basi atafanikiwa zaidi, bali kufanikiwa katika biashara kunategemea na mtu fulani anayefanya biashara iyo, kila aina ya biashara ina nafasi ya kukufanikisha kama utakuwa mtu sahihi kufanya biashara iyo.

Sababu ya pili ni KUKOSA MTAJI.

Waajiriwa wengi wameshindwa kuanzisha biashara nje ya ajira zao kwa sababu hawana mtaji wa kutosha kufanya hivyo.

Licha ya kuwa wanapata mshaara, bado wengi wao wamekuwa wanasema kwamba pesa wanayopata haitoshi hata kutimiza maitaji yao sasa inawezekanaje kuanzisha biashara na wakati pesa hakuna..

Ewe mwajiriwa inawezekana kabisa sababu hii ikawa na ukweli ndani yake lakini kwa kuendelea kuamini ivyo utakuwa unajichelewesha zaidi kufikia mafanikio yako, kwa sababu kwa wewe kuwa kwenye ajira una unafuu Sana wa kupata mtaji pesa hasa kama umedhamilia kweli kuanza biashara.

haijalishi unapata mshahara kidogo kiasi gani bado unaweza kutenga sehemu ya kipato chako na ukaitumia kama mtaji wa kuanza biashara, lakini pia kwa wewe kuwa kwenye ajira una nafasi ya kupata mkopo kutoka taasisi mbalimbali za kifedha na ukaweza kuanza biashara yako kwani ajira yako itatumika kama dhamana ya wewe kuweza kupata pesa kwenye taasisi izo.

Na hata kama utakuwa hauna mtaji pesa bado kuna biashara nyingi Sana unaweza kuanza kuzifanya bila hata ya kuwa na mtaji na ukajiongezea kipato.

Mfano unaweza kuanza kwa kufanya udalali yaani wewe unakutanisha pende mbili zenye uhitaji na wao wakishafanya biashara wewe unalipwa kamisheni kwa kuweza kuwakutanisha, lakini pia unaweza kuanzisha biashara yako kwa kutumia Imani ya wateja yaani wanakulipa kwanza pesa na wewe unawatafutia maitaji yao na unawapelekea na kubaki na faida.

yaani ukifungua kichwa utaona mambo mengi ambayo kwa sasa hauoni

Changamoto ya tatu ni KUKOSA MUDA WA KUSIMAMIA BIASHARA ZAO.

Ukiachana na changamoto ya wazo na mtaji wa biashara jambo lingine linalowasumbua waajiriwa wengi ni kukosa muda wa kusimamia biashara zao, na hili linatonaka na kuwa sehemu kubwa ya muda wa waajiriwa wengi wanautumia katika Kazi zao walizo ajiriwa..

Ni kweli kabisa ukiangalia sababu hii unaona inaukweli lakini kwa kuwa lengo ni kutafuta ukombozi na kuboresha maisha yako basi wewe mwajiriwa yakupasa kukabiliana na hili.

Ukweli ni kuwa licha ya kuwa Kazi yako imekubana Sana bado unaweza kupata muda wa kufanya biashara yako ya pembeni.

hili litawezekana kama tuu utaamua kuwa na matumizi mazuri ya muda wako wa ziada yaani badala ya kutoka Kazini na kurudi nyumbani kupumzika au kwenda vijiweni kupiga stori na marafiki wewe unatakiwa kutumia muda huu kuwekeza katika kufanya na kusimamia biashara yako.

ili siyo jambo jepesi ila linawezekana kabisa.

Kaa chini na angalia ni kwa namna gani unaweza kuwa na maisha ya siku mbili ndani ya siku Moja ( siku ya kwanza ikiwa ni ule muda wa Kazi na siku ya pili ikiwa ni ule muda wa ziada utakaoutumia kwenye biashara yako) kwa kufanya ivi lazima ufanikiwe.

Kama jambo hili litashindikana kwako basi unaweza kushirikiana na watu wengine na mkafanya biashara pamoja kupitia ubia au uwekezaji izo zote ni njia zitakazo kufanya wewe kuwa na biashara wakati umeajiriwa.

Ndugu yangu mpendwa izo ndiyo changamoto tatu kubwa zinazowasumbua watu wengi hasa walio kwenye ajira kushindwa kuanzisha na kufanya biashara nje ya ajira zao

Yawezekana hata wewe unayesoma hapa upo kwenye ajira na umekuwa unakutana na changamoto izo pale unapotaka kuanzisha biashara yako ya pembeni na umeshindwa ufanye nini ili kukabiliana nazo.

Naamini kwa kupitia somo ili umepata Mwanga kuwa inawezekana kabisa wewe kuwa na biashara nje ya ajira yako licha ya kuwepo kwa changamoto izi..

Basi kuanzia Leo anza kuamini kuwa inawezekana na fanyia Kazi SoMo hili ili uweze kuanzisha biashara yako.

Kama utaitaji msaada zaidi na muongozo wa wewe kuanza biashara ukiwa ndani ya ajira unaweza kuwasiliana nami kwa namba 0754818580 na nitakusaidia Sana.

Mungu akubariki Sana na akuwezeshe kuanza biashara nje ya ajira yako ili uweze kununua uhuru wako

Nenda kafanikiwe


Posted

in

by

Tags:

Comments

2 responses to “Sababu kuu tatu kwa nini waajiriwa wengi wameshindwa kuanzisha biashara nje ya ajira”

  1. Teknik Informatika Avatar

    Je, unakubaliana na wazo la kuanzisha biashara za pembeni nje ya ajira kama njia ya kupata uhuru wa kifedha na kupiga hatua kubwa zaidi kwenye maisha? Kwa upande bora Telkom University

    1. Mwl Baraka Avatar

      Kabisa na hii ndiyo njia ya uhakika ambayo unauwezo wa kumpa mtu kipato kisichokuwa na ukomo.

      Kwani kupitia biashara unaweza kupanga ni kiasi gani uingize kwa siku, wiki, mwezi au mwaka. Tofauti na ilivyo kwenye ajira ambapo licha ya kuweka juhudi kubwa kwenye Kazi na uzalishaji bado huna mamlaka ya kuamua ni kiasi gani cha kipato ulipwe

      Mtu mwingine ambaye ndiyo bosi wako ndiye anayeamua wewe ulipwe shs ngapi kwa Kazi unayofanya

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *