Jenga vyanzo vingi vya mapato

Maisha ya mwanadamu hayawezi kuwa na maana na yenye furaha bila kuwa na uwezo wa kifedha

kutokana na sababu hii kubwa na ya msingi

Kila mtu amekuwa akiamka asubuh na mapema kwenda huku na kule kufanya Kazi kwa bidii ili aweze kupata pesa,kwani kupitia pesa ndiyo mwanadamu anaweza kutimiza maitaji yake

hii ni kwa sababu pesa ndiyo nyenzo kuu ya mabadilishano baina ya watu na watu na utumika kama kipimo cha thamani. Ivyo ili uweze kupata chochote unachotaka kwenye maisha lazima uwe na pesa.

Huu ndiyo ukweli ulio wazi kabisa kwamba bila pesa uwezi kuwa na maisha yenye maana.

Licha ya wengi kuwa na kauli kwamba pesa siyo kila kitu maishani lakini bado ukweli utabaki palepale kuwa uwepo wa pesa unasababisha mambo mengi Sana kuwezekana

kupitia pesa utaweza kupata maitaji yako muhimu kama vile chakula, mavazi, malazi, matibabu, kujifunza, kusafiri, kumiliki Mali, na mambo mengine mengi yaletayo furaha

Sasa kwa kuwa tumeona jinsi pesa ilivyo muhimu basi tunatakiwa kuwa nazo nyingi Sana kwani bila kufanya ivyo maisha yetu hayatakuwa vile tutakavyo

Na ili kuondoa matatizo ya kifedha maishani mwetu tunalazimika kuwa na vyanzo vingi Sana vya mapato.

watu wengi sana wamekuwa na changamoto ya kuwa na chanzo kimoja tu cha mapato jambo ambalo limeendelea kuwatesa na kuwanyima fursa ya kufurahia maisha watakavyo

hii ni kutokana kuwa chanzo kimoja cha mapato siku zote ni kifungo kinacho kufanya usiishi maisha yako vile utakavyo na kukosa uhuru.

kwani kila kitu utakachotaka kufanya kwanza yakupasa utazame una nini mfukoni mwako,

na kama bajeti yako haitoshi basi ni wazi kuwa hautaweza kufanya baadhi ya mambo ya muhimu kwa sababu ukithubutu kufanya utajikuta unaingia kwenye matatizo makubwa ya kifedha.

Sasa kwa kuwa kila kukicha matumizi na maitaji yetu yanaongezeka, mtu mwenye chanzo kimoja cha kipato anazidi kuchanganyikiwa na kujiona kama yeye hana bahati katika dunia hii.

Na kwa kutambua ilo ndiyo maana ninakuandikia Makala hii ili uweze kuona umuhimu wa vyanzo vingi vya mapato na uondoke kwenye icho kifungo cha kujitakia na ununue uhuru wako.

Ukweli ni kwamba mwanadamu ili aweze kuwa na uhuru juu ya maisha yake anatakiwa kuwa na uwezo wa kupata maitaji yake yote bila wasiwasi na kwa kuwa maitaji ya mwanadamu hayana ukomo utaweza kuyapata kwa kuwa na vyanzo vingi vya kipato.

kwa kujenga vyanzo vingi vya mapato utakuwa na nguvu kama bahari kwani haijalishi jua litakuwa Kali na litawaka kwa muda mrefu kiasi gani bado utakuwa na maji ya kutosha.

vyanzo vingi vya mapato vitakupa kujiamini na kuweza kuishi maisha utakayo. Hautakuwa na mtu wa kukuyumbisha na kukusumbua maishani kwani utakuwa na uwezo wa kumudu maisha yako kwa kiasi kikubwa.

Mwenye vyanzo vingi vya mapato ndiyo mwenye uhuru wa kweli kwani ana uwezo wa kupata maitaji yake yote na kwa wakati wowote

lakini pia anauwezo wa kusaidia watu wengine na kuwezesha mambo mengine mengi kuweza kufanikiwa.

Kumbuka chanzo kimoja cha mapato ni utumwa na hakuna uhuru kabisa na kama mapaka sasa unaamini uko salama jua unajidanganya

Kwani kama kikitokea cha kutokea kwenye shughuri yako unayofanya iwe ni Kazi, biashara au kwenye afya yako na ukashindwa kuendelea na uzalishaji tambua kuwa kipato chako nacho kitakoma na maisha yako yatakuwa magumu zaidi.

Zingatia uhuru wa maisha upo kwenye vyanzo vingi vya mapato na tafiti zinaonyesha watu wote wenye mafanikio makubwa na wanaofurahia maisha Yao Wana wastani wa vyanzo vinne mpaka Saba vya mapato. Vipi kuhusu wewe

ivyo ni wakati wako kushituka na ku tambua umuhimu wa vyanzo vingi vya mapato na anza kuvijenga vyanzo hivyo ili uweze kukomboa maisha yako.

naamini umejifunza kitu na utakwenda kuweka katika matendo

kama utaitaji ushauri wa karibu zaidi wasiliana nami kwa namba 0754818580

nitakusaidia ni namna gani na wewe unaweza kununua uhuru wako kwa kuanzisha vyanzo vingi vya mapato

Mungu akubariki kwa kuwa utafanyia Kazi hekima hizi.

nenda kafanikiwe.


Posted

in

by

Tags:

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *