Utumwa wa chanzo kimoja cha mapato kwa waajiriwa wengi

Ndungu yangu mpendwa.

watu wengi waliojiriwa wana changamoto moja kubwa Sana ambayo ina wakosesha furaha na kushindwa kupiga hatua kwenye maisha yao

licha ya kuwa katika jamii zetu aliye ajiriwa anaonekana ni mtu ambaye ana mafanikio na amepiga hatua kuliko wale ambao hawapo kwenye ajira,

bado waajiriwa wengi wanapitia mateso na taabu kubwa kwa sababu ya changamoto ya kutokuwa na kipato kinacho watosheleza

waajiriwa wengi duniani ikiwa ni pamoja na hapa Tanzania ni watu ambao wanategemea chanzo kimoja cha kipato

Mshahara wanaolipwa kila mwisho wa mwezi kupitia Kazi mbalimbali wanazofanya ndiyo chanzo pekee cha mapato wanacho kitegemea kwa ajili ya kuendesha maisha yao.

Chanzo kimoja cha kipato ndiyo mtego ulio tegwa kupitia ajira na umeweza kunasa maisha ya waajiriwa wengi na kuwafanya kuendelea kuwa watumwa kwa Kazi zao miaka nenda miaka rudi.

Hakuna mtu aliyefikia mafanikio ya juu kwenye maisha na kuwa tajiri kwa kutegemea mshahara peke yake.

Waajiriwa wengi wameendelea kuwa masikini na kuishi maisha duni kwa sababu kipato wanachokipata kinaishia kwenye kulipa gharama ya matumizi wanaokuwa nayo.

haijalishi mtu analipwa kiasi gani cha pesa kupitia Kazi anayofanya bado watu hawa wanakabiliwa na changamoto ya matumizi kuwa mengi zaidi ya kipato chao

Watu wote walio kwenye ajira kuna namna wanavyo chukuliwa katika jamii na familia zao kwa ujumla jambo linalopelekea watu hawa kubeba mzigo mkubwa Sana ki matumizi kupitia chanzo kimoja cha mapato walichonacho

kuna matumizi yanayo wahusu wao binafsi, kuna matumizi ya familia zao, kuna matumizi yanayotokana na Kazi zao, kuna matumizi ya kijamii na mengine mengi yote haya yanatazama kwenye icho kipato kimoja .

Pia waajiriwa wengi wanashindwa kupiga hatua kubwa kwa sababu licha ya kuwa matumizi Yao na maitaji Yao ni mengi na Yana endelea kukua kila siku bado kipato chao hakiongezeki kabisa

hali hii imewafanya wengi wao kujikuta wakiangukia kwenye shimo kubwa Sana la mikopo na kuishia kuwa na madeni chungu nzima wakitafuta kunusulu maisha Yao.

Aliye ajiriwa Hana maamuzi ya kupanga ni kiasi gani atalipwa kila mwisho wa mwezi kwa Kazi aliyofanya, badala yake yupo mtu mwingine ambaye anapanga yeye alipwe kiasi gani hata kama atafanya Kazi kwa bidii Sana.

Uwepo wa mtu mwingine anayepanga kipato chako ndiyo ukomo uliowekwa Kwa mwajiriwa kuweza kupiga hatua kwenye maisha yake licha ya bidii anayoionyesha kwenye Kazi.

Ndugu yangu uliye kwenye ajira ni dhahiri umeona kuwa ni jinsi gani mshahara wako hauwezi kukuletea mafanikio makubwa unayo tamani kuwa nayo maishani mwako.

na umekuwa unapitia changamoto hii miaka mingi kwenye maisha yako licha ya jamii na watu wa karibu kuona kama wewe ni mtu uliyefanikiwa kwa sababu una Kazi yenye kipato cha uhakika.

Leo kupitia Makala hii nakuakikishia kuwa licha ya kuwa una Kazi ya kipato cha uhakika

uwezi kufanikiwa kwa viwango vya juu zaidi kwa kutegemea mshahara pekee hivyo nataka ushike hatamu juu ya maisha yako kwa kutafuta namna ya kuanzisha vyanzo vingine vya kipato.

Ukweli ni kuwa waliofanikiwa wote huwa Wana wastani wa vyanzo vinne mpaka Saba vya mapato jambo linaowafanya waweze kuwa na uhuru wa kipato na kufurahia maisha yao.

Hata wewe yakupasa uanze kufikiri juu ya kuongeza vyanzo vingine vya mapato ili uweze kunufaika.

bahati nzuri ni kwamba unaweza kufanya ivyo sasa bila hata kuacha Kazi yako unayofanya.

Zungatia kuwa chanzo kimoja cha kipato kitakufanya wewe kuweza kuishi maisha ya kawaida lakini kwa kujenga vyanzo vingi vya mapato utaweza kufanikiwa zaidi.

asante kwa kuwa umejifunza na naamini utakwenda kufanyia Kazi SoMo ili kwa kuanza kujenga vyanzo vingine vya mapato.

kwa msaada zaidi wasiliana nami kwa namba 0754818580

huu ni wakati wa kutafuta uhuru wako wewe uliye kwenye ajira.

Nenda kafanikiwe


Posted

in

by

Tags:

Comments

2 responses to “Utumwa wa chanzo kimoja cha mapato kwa waajiriwa wengi”

  1. Teknik Telekomunikasi Avatar

    Je, unaona ni njia gani nzuri au suluhisho gani linaweza kutolewa ili kusaidia waajiriwa kukabiliana na changamoto ya kutokuwa na kipato kinachowatosheleza na hivyo kuishi maisha bora zaidi? Kuhusu Telkom University

    1. Mwl Baraka Avatar

      Njia nzuri ambayo ninapendekeza ili kuwasaidia waajiriwa wengi kuondokana na changamoto ya kipato kutokutosheleza ni wakati sasa wa waajiriwa kujifunza kuhusu ujasiliamali na kutumia muda wao wa ziada kufanya biashara zitakazo waingizia kipato cha ziada lakini pia waajiliwa wengi hawana elimu kuhusu uwekezaji na faida wanazoweza kupata kwa kujihusisha na uwekezaji.

      Hivyo wanapasa kujifunza pia na kuanza kuwekeza kwa kufanya hivi wataweza kujenga vyanzo vingi vya mapato kitu ambacho kitapelekea wao kufikia uhuru wa kifedha

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *