Fikiri kwa ukubwa ili ufanikiwe

Moja ya sababu kubwa iliyowafanya wale waliofanikiwa kuweza kufanikiwa zaidi katika maisha yao ni uwezo wao wa kufikiri kwa ukubwa na upana.

kufikiri kwa ukubwa na upana kunatoa nafasi ya kuisukuma akili kulazimika kufanya mambo ambayo kwa kawaida ni ngumu kwa mtu kuweza kufanya.

hii ni kutokana na kuwa sisi wanadamu huwa tunauwezo mkubwa Sana ndani yetu, uwezo wa kufanya maajabu makubwa kama tukitumia akili zetu sawasawa.

Lakini tumekuwa hatuwezi kufanya ivyo kwa sababu hatujailazimisha akili yetu kufikiri kwa mapana

sasa ili uweze kufikia mafanikio makubwa unatakiwa uanze kwa kuwa na fikra Pana na ufikiri kwa ukubwa

Kaa chini na waza mambo makubwa unayotamani kuwa nayo katika maisha yako

Haijalishi ukubwa wa kitu unachofikiri ndani yako wewe fikiri kuhusu kitu icho kwa ukubwa na utafanikiwa kukitimiza.

kwa wewe kuwa na ndoto kubwa unayotamani kuitimiza katika maisha yako ndiko kutaifanya akili yako kuweza kujisukuma kuja na njia mbalimbali zitakazo kuwezesha kufanikiwa

Hata siku Moja usikubali kuyafunga maisha yako kwa mawazo madogo.

Hata siku Moja usiruhusu hali yako ya sasa iamue hatima ya maisha yako.

Anza kubadili maisha yako kwa kufikiri kwa mapana

kumbuka aonavyo mtu nafsini mwake ndivyo alivyo.

Hii ina maanisha kuwa kama kupitia fikra zako unajiona wewe ni mtu mdogo basi ndivyo utakavyo kuwa, na kama unajiona wewe ni mtu mkubwa uliyefanikiwa pia ndivyo utakavyo kuwa..

Zingatia hakuna gharama kubwa utakazolipa kwa kufikiri kwa mapana na kwa ukubwa juu ya maisha yako

Gharama utakazotumia kufikiri mawazo madogo juu ya maisha yako ndiyi gharama izoizo utakazotumia kufikiri kwa mapana na kwa ukubwa.

ivyo ni Bora kufikiri kwa mapana kwani dunia itakupa sawasawa na kile unachokifikiria.

Leo amua kuanza kufikiri kwa ukubwa na kutengeneza fikra kubwa kuhusu Maeneo mbalimbali ya maisha yako na utaona jinsi utakavyofanikiwa zaidi.

Hongera Sana kwa kuwa umejifunza.

Fanyia Kazi SoMo ili na utafanikiwa.

Nenda kafanikiwe.


Posted

in

by

Tags:

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *