Usirudie makosa Aya kwa mwaka 2024

Ndugu yangu mpendwa heri ya mwaka Mpya

leo ikiwa ni siku nyingine na mwaka mwingine wa 2024 ambao Mungu ametupa kama zawadi ninataka nikushirikishe mambo muhimu Sana ambayo kama utayafanyia Kazi yatakwenda kubadirisha maisha yako kabisa

ni kweli umekuwa na mwaka mzuri Sana wa 2023 pamoja na miaka mingine iliyopita

katika miaka iyo uliweza kufanya mengi na uliweza kufanikiwa katika mengi lakini uliweza kuanguka na kushindwa katika mengi pia.

Na inawezekana kuna mambo mengi mazuri ambayo ulishindwa kuyafanikisha kwa sababu ya uzembe na tabia zako, yote hayo yameshapita. kwa mwaka huu yakupasa kubadilika na kuacha kuishi kwa mazoea tena

sasa kupitia Makala hii ninakwenda kukupa mambo matatu makubwa ambayo pengine yalikuwa ni makosa uliyoyafanya kwa mwaka 2023 na miaka mingine iliyopita. Na sitaki uyafanye tena kwa mwaka huu wa 2024 na miaka inayokuja ili maisha yako yaweze kuwa na maana na uweze kutimiza ndoto Zako.

Makosa ambayo sitamani uyarudie tena ni haya hapa.

  1. KUISHI MAISHA YASIYO NA MALENGO.

Ndugu yangu mpendwa maisha tunavyoishi katika dunia hii ni maisha ya malengo.

wewe ulikuja duniani kukamirisha lengo Fulani. Ivyo katika maisha yako yakupasa uwe na malengo

Watu wengi sana wamekuwa wanaishi bila malengo yaaani wao wanakuwepo tu wakisogeza siku bila kuwa na mambo ya msingi wanayofanyia Kazi,

Kwa mwaka huu wa 2024 ukitaka maisha yako yabadilike Kaa chini na weka malengo. Kamwe usikubali kurudia kosa ulilolifanya mwaka 2023 la kuishi na kuendesha maisha yako bila kuwa na malengo.

Kaa chini na andika nini unataka kufanikisha katika maisha yako hasa kwa mwaka huu, andika ni mtu wa namna Gani unatakiwa kuwa kwa mwaka huu, andika ni tabia za namna gani unakwenda kuzijenga kwa mwaka huu. Andika mambo yote unayotaka kuyatimiza katika maisha yako na yapange kwa vipaumbele.

unapokuwa na malengo unakuwa na dira kwani malengo ni ramani inayoongoza maisha yako. Inakuonyesha ulipo sasa na wapi unataka kwenda na jinsi ya kufika uko.

ivyo basi Kaa chini na tengenenza malengo katika kila eneo la maisha yako kuanzia, familia, wewe mwenyewe, Mali unazotaka kumiliki, Malengo juu ya Imani yako, malengo juu ya biashara, malengo juu ya fedha, malengo juu ya uwekezaji na malengo juu ya afya yako.

2. KUTOKUJIFUNZA NA KUJIELIMISHA KILA SIKU .

kosa la pili ambalo sitamani ulifanye tena kwa mwaka 2024 ni hili la kutokujifunza na kujielimisha kila siku.

Ndugu yangu mpendwa dunia tunayoishi sasa ni dunia ya taarifa na maarifa. Mambo yanabadilika Sana, kile kilicho kuwa kweli Jana inawezekana kikawa hakiko ivyo Leo, na kile ulichotegemea kwamba kitakuwezesha kuishi Leo inawezekana kisifanikiwe kukusaidia kwa sababu mambo yamebadilika.

Sasa kama hautakuwa tayari kuendana na Kasi ya mabadiliko haya uwe na uhakika kabisa kuwa utaachwa nyuma.

Kama kwa miaka iliyopita ulikuwa ni mtu wa kuchukia maarifa na taarifa sahihi basi mwaka huu tafuta maarifa ili uwe bora zaidi kwani kupitia kujifunza ndiyo unaweza kukutana na mambo ya kufungua akili yako na kuleta badiliko maishani mwako

Achana na mambo ya kujifanya unajua kila kitu. Kuwa mpole kubali kujifunza kutoka kwa watu mbalimbali na kama utafanya ivyo utapata mambo mengi Sana na utakuwa na mafanikio makubwa Sana kwenye maisha yako

jifunze na jifunze na jifunze tena hasa kwa kuwasikiliza watu, kusoma vitabu na kujifunza kupitia mafunzo yaliyo kwenye mitandao hasa mtandao wa YouTube kwani kupitia kule utapata masomo ya jambo lolote UNALOTAKA kulijua na utabadilisha maisha yako kabisa.

3. KUTOKUWA NA UWEKEZAJI KWA AJILI YA BAADAE.

ndugu yangu mpendwa jambo la tatu ambalo pengine ni kosa umelifanya kwa miaka ya nyuma ukiwepo mwaka 2023. Ni kuishi bila kufanya uwekezaji.

kosa ili linaweza kuwa limesababishwa na wewe kukosa elimu juu ya uwekezaji au pengine umekuwa na Imani potofu juu ya uwekezaji

sasa kwa mwaka huu natamani Sana uanze kufanyia Kazi swala hili. Tafuta maarifa sahihi kuhusu uwekezaji, jifunze na anza kuwekeza hii ni muhimu Sana na utapata manufaa makubwa Sana kama utafanyia Kazi

Inawezekana ukawa ujui uwekezaji ni nini, faida zake ni zipi na ni Maeneo gani unatakiwa kufanya uwekezaji. Ilo sisikupe taabu Mimi ninatoa elimu juu ya eneo ili na kama utataka kujifunza zaidi karibu nitakufundisha.

Sasa kwa kuwa uwekezaji ni muhimu kuna eneo moja ambalo natamani ulifanyie Kazi mwanzoni mwa mwaka huu kwa kutafuta maarifa yake na taarifa na uanze kuweza mara moja na eneo lenyewe ni uwekezaji wa kununua Vipande katika Mifuko ya uwekezaji wa pamoja na bahati nzuri ni kwamba kwa Tanzania kuna taasisi inayohusika na uwekezaji huu inayoitwa UTT AMIS. Ambayo unaweza kufanya uwekezaji na ukanufaika Sana

Hayo ndiyo mambo matatu ambayo sitamani uyarudie tena kwa mwaka huu wa 2024.

na kama utaitaji msaada katika maeneo hayo matatu unaweza kuwasiliana na Mimi moja kwa moja kwa namba 0754818580 na nitakusaidia jinsi ya kufanyia Kazi maeneo haya na yatabadilisha maisha yako kabisa

Mungu akubariki Sana kwa kujifunza

Nakutakia mafanikio makubwa Sana kwa mwaka 2024

Nenda kafanikiwe.


Posted

in

by

Tags:

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *