Iki ndicho kinakufunga na kukuzuia kufanikiwa zaidi.

Ndugu yangu mpendwa moja ya kitu ambacho kimekwamisha watu wengi na kitaendelea kukwamisha watu wengi kufikia mafanikio makubwa zaidi kwenye maisha Yao ni

AJIRA NA MAISHA YA MSHAHARA

Inawezekana ukawa umeshangazwa na kauli hii kwamba ajira na maisha ya mshahara ni kikwazo cha mafanikio makubwa kwa watu wengi kwenye maisha, kwa sababu umekuwa ukiamini kuwa walio na Ajira tayari wametoboa kwenye maisha.

Kupitia makala hii nitakueleza ni kwa nini iko ivyo

Ndugu yangu ni kweli kabisa kuwa ajira na mshahara ndiyo tegemeo la watu wengi na watu wengi ambao Wana ajira na wanapokea mshahara kila mwisho wa mwezi wanaonekana kuwa na uhakika wa maisha kwani wanaweza kuyaendesha maisha yao na kupata maitaji yao ya muhimu.

Pia ni ukweli usio pingika kuwa kuna watu wengi wameweza kupata mafanikio makubwa kutokana na ajira zao kuwa na mshahara mkubwa pamoja na nafasi kubwa ya kutengeneza kipato kupitia marupurupu mbalimbali yanayotokana na aina ya ajira zao lakini ni asilimia ndogo Sana ya watu walio kwenye kundi hili.

Watu wengi walio ajiriwa kipato chao ni cha wastani na wengine bado kipato chao ni kidogo Sana ambacho akiwezi kutosheleza kumudu gharama za maisha.

Ndugu yangu Ajira inakutaka utoe muda wako, nguvu zako na ujuzi wako kufanya Kazi na mwisho wa siku ulipwe kwa Kazi uliyoifanya.

Ajira ni kikwazo kwa mafanikio ya watu wengi kwa sababu Watu wengi wanategemea ajira pekee kama njia ya kuwaingizia kipato na wanatumia muda mwingi wakiwa katika Kazi na kushindwa kujihusisha na shughuri nyingine ambazo zingewaingizia kipato na kuwawezesha kupiga hatua kubwa kwenye maisha yao.

Pia ajira Ina ukomo wa kipato ambacho mtu anaweza kupata kutokana na Kazi aliyofanya,

Ukomo huu wa kipato ndiyo mateso na kifungo kikubwa kwa mafanikio ya watu wengi kwani licha ya kufanya Kazi kwa bidii katika ajira zao bado hawawezi kupanga ni kipato kiasi gani walipwe yaani bado kuna mtu mwingine ndiye ataamua wewe ulipwe kiasi gani jambo ambalo halitakufikisha kwenye uhuru wa kifedha .

Ajira na maisha ya mshahara ni kikwazo kwa mafanikio makubwa kwenye maisha ya watu wengi kwa sababu kipato unachopata kwenye maisha yako kinakuwezesha wewe kuweza kuishi na kulipia gharama za maisha tu na siyo kufanya uwekezaji na biashara.

Kwa watu wengi walio kwenye ajira kipato wanachopata ni kidogo Sana na hakitoshelezi hata kumudu gharama za maisha yaani kama unategemea Kazi ya kuajiriwa pekee kuendesha maisha yako na kama una familia bado maisha yako nayaweza kuendelea kuwa magumu.

licha ya kuwa una unafuu ukilinganisha na asiye na njia nyingine ya kuingiza kipato na iki kinakuwa kikwazo cha wewe kufanikiwa zaidi kwa sababu kipato chote kinaishia kwenye matumizi.

Lakini pia Ajira na maisha ya mshahara yanakufunga kufikia mafanikio makubwa kwenye maisha yako kwa sababu kunakufanya uishi kwa kutegemea mshahara tu.

Akili yako inafungwa kwenye kufikiria kuhusu ajira peke yake na unakuwa hauoni fursa nyingine ambazo zinaweza kukuingizia pesa zaidi.

Pia maisha ya Ajira na mshahara yanakufanya ushindwe kufurahia maisha yako kwani chochote unachotaka kufanya kwenye maisha yako utalazimika kukifanya kulingana na bajeti ya kipato chako na kama kipato chako hakitoshelezi uwezi kufanya mambo unayoyapenda kwa sababu mshahara umekufunga.

Ndugu yangu mpendwa inawezekana hata wewe ulikuwa unaona ajira na mshahara unaopata kama ni mkombozi wa maisha yako. Lakini kupitia Makala hii umeona kuwa ajira na mshahara vina ukomo na kupitia ivyo uwezi kupata mafanikio makubwa kwenye maisha yako.

Sasa nini kifanyike

Ikiwa uko kwenye ajira na unapokea mshahara yakupasa ujue kwamba wewe una bahati Sana kwani tayari una njia ya kukuingizia kipato ambacho kitakuwezesha kulipa gharama za maisha yako ya kila siku

lakini ili kufanikiwa zaidi na kufikia mafanikio makubwa hautakiwi kutegemea ajira yako peke yake, badala yake unatakiwa utafute namna nyingine ya kuingiza kipato kupitia kufanya biashara na uwekezaji.

kwani kwa kufanya biashara na uwekezaji hakuna ukomo wa kipato na unaweza kuingiza kipato kikubwa uwezavyo na kufikia mafanikio makubwa zaidi kwenye maisha yako.

leo kupitia Makala hii naomba uondoke na ujumbe huu kuwa ajira na mshahara havita kufikisha kwenye mafanikio makubwa zaidi kwa sababu ajira Inakupa kipato chenye ukomo.

Na ukitaka kufikia mafanikio makubwa zaidi kwenye maisha yako yakupasa ujenge mifereji mingi ya kipato kupitia Biashara na Uwekezaji…..

Niandikie kwenye comment nini umejifunza kwenye somo ili na ni kitu gani umepanga kufanya kama njia ya pembeni ya kuingiza kipato zaidi

Na kama utaitaji ushauri na muongozo wa aina gani ya biashara ufanye na muongozo wa maeneo ya uwekezaji usisite kuwasiliana nami kupitia

0754818580

Mungu akubariki Sana kwa kujifunza

Nenda kafanikiwe.


Posted

in

by

Tags:

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *