Usumbufu namba moja kwa Karne ya 21

moja ya kitu kikubwa kufanyika kwa mafanikio makubwa katika Karne ya 21 ni mapinduzi makubwa Sana ya ki teknologia.

Kupitia ukuwaji huu wa teknologia tumeona mambo mengi Sana yamebadilika katika nyanja mbalimbali za maisha kuanzia, uchumi, uchukuzi, viwanda, biashara, Kazi na Huduma mbalimbali katika jamii.

kila kitu sasa kinafanyika kwa urahisi zaidi kwa kutumia teknologia na uzalishaji umekuwa mkubwa Sana.

licha ya faida nyingi Sana ambazo zinatokana na teknologia katika maisha yetu bado kuna madhara mengi Sana ambayo yanatukumba sisi wanadamu ikiwa ni kwa kujua au kwa kuto kujua.

Na Moja ya jambo kubwa Sana ambalo limekuwa tatizo kwa maisha ya watu wengi kwa sasa ni matumizi yasio sahihi ya simu za mkononi hasa izi simu janja maarufu kama smartphone.

Simu janja ndiyo imekuwa usumbufu mkubwa Sana kwenye Karne ya sasa kwa sababu inakufanya umiliki dunia yote kiganjani mwako.

Na kwa kuwa watu wengi hawajui matumizi sahihi ya utandawazi na utumiaji wa smartphone kwa manufaa hali inazidi kuwa mbaya zaidi kwani watu wengi tunatumia simu izi ndivyo sivyo na kwa kuwa waliotengeneza simu izi wamejua nini hasa watu wanapenda basi ndiyo wanatumia mwanya huo kuwalisha taarifa na habari mbalimbali zitakazo kusisimua na kukufurahisha ili uendelee kuzamia uko.

Smartphone Ina mambo mengi Sana, na nguvu kubwa inayoifanya Smartphone kuwa na nguvu kubwa ni uwepo wa internet ambayo inakuwezesha wewe kuperuzi na kuona mambo yote Kona zote za dunia bila kujali mambo hayo Yana manufaa kwako au yanakuharibu.

kupitia smartphone unaweza kujifunza mambo mbalimbali na kuwa na maarifa mengi yatakayokusaidia kwenye maisha yako.

lakini watu wengi hawafanyi ivyo kwa sababu kufanya ivyo kuna boa yaani kushika simu na kuanza kusoma taarifa za kujenga au kusikiliza na kuangalia video ya mafunzo yenye manufaa ni Kazi sana na inachosha akili na mwili kwa wengi kwa kifupi inakela.

badala yake watu wengi wanatumia smartphone izi kwa kujiburudisha na kujifurahisha tu

na kwa kuwa jambo hili la kujifurahisha na kuburudika ndilo limekuwa itaji la wengi. Watu wamekuja na njia mbalimbali za kukufanya ufurahi kupitia mitandao ya kijamii

yaani kupitia Facebook, Instagram, YouTube, tick-tock, WhatsApp na mitandao mingine ya kijamii unayoifahamu watu wanatumia ujinga wa watu wengine kutengeneza kipato kwa kutoa taarifa na maarifa ambayo ni ya kufurahisha na kuburudisha ili uendelee kufatilia na kufurahia bila kujua kuwa unajiibia muda wako ambao ungetumia kufanya mambo mengine yenye tija

katika dunia ya sasa ni ngumu Sana mtu kukaa kwa dakika kumi bila kushika na kuangalia kinachoendeea kwenye simu yake ya mkononi. Yaani ukisikia tu ki message kimeingia umechungulia, ukisikia ki kengele kimelia umechungulia na pia hata bila kusikia chochote umekuwa utamaduni kuchungulia.

Huu ni usumbufu mkubwa Sana kwa maisha ya watu wengi sana kwa dunia ya sasa.

Smartphone imekuwa mwizi mkubwa Sana wa muda wa watu wengi, imechukua umakini wa watu wengi sana kwenye maisha yetu.

popote unapokuwa watu wako bize na simu za mkononi. Iwe ni nyumbani Wana familia hawazungumzi kila mtu Yuko bize kainamia simu yake kibaya zaidi tunaenda na simu izi mpaka kitandani na tunatumia kabla ya kulala na tunapoamka ndiyo kitu cha kwanza kuanza nacho.

Nenda kwenye maeneo ya Kazi ufanisi unapungua kwa sababu ya simu za mkononi, muda wa Kazi watu badala ya kufanya Kazi wao wako bize na simu zao kwenye mitandao ya kijamii.

Hata safarini saivi ni balaaa yaani mnaweza kuwa kwenye gari ukashangaa ukimya umetawala ndani ya gari ukiangalia hakuna kinachoendeea zaidi ya watu kuwa bize kwenye simu zao za mkononi.

Hakika huu ni usumbufu hasa na tusipo angalia na kuchukua hatua stahiki mambo yataendelea kuwa mabaya.

Ndugu yangu mpendwa

naomba nimalize Makala hii kwa kukwambia kuwa smartphone zimekuwa na usumbufu mwingi Sana na kwa kuwa mambo mengi na taarifa nyingi zilizo kwenye simu izi ni za kutupa Raha na furaha zimewafanya watu wengi sana kuwa waraibu ( addicted) wa matumizi wa simu na kushindwa kujizuia.

Kwa wewe kujifunza kupitia somo ili naomba usiingie katika addiction ya matumizi ya simu kwa kuanza kuwa na mipaka katika matumizi yako ya simu hasa smartphone.

kwa kufanya ivi utakuwa umeepuka usumbufu mkubwa Sana kwenye maisha yako.

Niandikie kwenye comment ni kwa namna gani smartphone imekuwa usumbufu kwako na tutajadiliana namna Bora ya kutatua tatizo ilo.

Mungu akubariki Sana kwa kujifunza

Nenda kafanikiwe.


Posted

in

by

Tags:

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *