Iki ndicho kitatokea kwa watu wengi miaka 20 ijayo

Ndugu yangu mpendwa

Kitu chochote ambacho hukukifanya Leo katika maisha yako, iwe ni kwa kujua au kuto kujua miaka 20 baadae utajilaumu Sana kwa kutokukifanya pengine utajutia Sana na Wenda usijisamehe kabisa.

Watu wengi tumekuwa na tabia ya kughairisha mambo muhimu Sana kwenye maisha kwa kuona kama muda sahihi wa kufanya bado haujafika….

……Lakini wakati mwingine tumekuwa tukijifariji kwamba mambo bado hayajakaa sawasawa na tutaanza kufanya kesho.

Mpendwa nina uhakika mpaka sasa kuna mambo mengi Sana yapo ndani ya moyo wako na umekuwa ukiyafikiria kila siku na unatamani kuanza kuyafanyia Kazi ila kila ukifikiri unaanzaje unaona ugumu na kuamua kuacha kufikiri

Iyo hofu inayokuzuia inakudanganya na kama hautaipinga na kuikataa itakutesa na kukuibia maisha yako yote..

..Yaani unaamini kwamba ukianza kufanya watu watakucheka, watu watakusema vibaya, watu watakukataa na wakati mwingine unaona kushindwa hata kabla ujaanza.

Huo ni mtego na unatakiwa kuutegua bila ivyo miaka 20 baadae utajijutia Sana pale maisha yako yatakapokuwa magumu zaidi ya yalivyo sasa,kwa sababu ukuchukua hatua Leo kwa kuogopa hofu.

Nikwambie tu jambo moja yale yote unayohofia huwa hayatokei na kwa baadhi ya yanayotokea huwa yanatokea kwa sababu ambayo ni kukuvusha kwenda hatua inayofata.

Usikubali kushindwa kabla ya kuanza, usikate tamaa kabla ya kujaribu , usiumize moyo wako kwa mawazo yasiyokuwa na utekelezaji hayo ni mateso unajipa na unaharibu afya yako.

Leo amua kuchukua hatua .Amini inawezekana, Amini unaweza kupata kile unachotamani kukipata, amini unaweza kufikia mafanikio na kutimiza malengo uliyonayo. Amini unaweza bila wasiwasi.

Kumbuka kama kuna watu wengine waliweza kufanya kile ambacho unatamani kufanya iyo ni ishara nzuri Sana kwamba inawezekana hata kwako…..

…… Na kama kuna kitu unatamani kufanya na hakuna mtu aliyewai kufanya akafanikiwa jua iyo ni ishara nzuri zaidi kuwa wewe ndiyo unatakiwa kuwa wa kwanza kufanikiwa kufanya icho ili uvunje rekodi.

Inawezekana

Jipe nguvu na anza kupigania unachokiamini.

Usikubali kuwa mtu mwenye majuto miaka 20 ijayo kwa sababu tu umekuwa unaghairisha mambo muda huu.

leo amua kuchukua hatua ya kuanza icho unachotamani kukifanya na utaona jinsi mawazo yako yalivyo kuwa yanakudanganya.

Mungu akuongoze katika kutimiza ndoto Zako na nakutakia utekelezaji mwema

nenda kafanikiwe


Posted

in

by

Tags:

Comments

2 responses to “Iki ndicho kitatokea kwa watu wengi miaka 20 ijayo”

  1. Telkom University Avatar

    Je, kuna jambo lolote ambalo unalijua au unalifikiria leo ambalo unakiri kwamba kama hutalifanya, miaka 20 kutoka sasa utajilaumu sana au kutajuta? Tembelea sisi Telkom University

    1. Mwl Baraka Avatar

      Ndio na jambo lenyewe ni kutokujifunza mambo mapya

      Ikiwa kama Leo hii hautakuwa tayari kujifunza mambo mapya ambayo yatakupatia ujuzi na ufahamu mpya wa kufanya mambo na kuziona fursa mbalimbali zinazokuja katika maisha yako

      Basi ni dhahiri kuwa miaka 20 baadae utakuwa na majuto makubwa Sana kwani ni elimu pekee na utayari wa kujifunza ndiyo unaweza kukufungulia dunia yako

      Na ninaposema elimu si maanishi elimu ya darasani pekee Ile inayopatikana kwa njia rasmi Bali nina mtaka mtu awe tayari kujiendeleza katika elimu ya Maendeleo binafsi kwani kupitia hii ataweza kutambua uwezo mkubwa pamoja na vipawa na karama zilizo ndani yake na namna gani ya kuzitumia kimafanikio.

      Lakini pia atakuwa na uwezo wa kuziona fursa na kuzichangamkia kitu ambacho kitamletea mafanikio makubwa Sana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *