Mambo matatu unayoyaitaji ili kufikia mafanikio ya juu zaidi kwenye maisha yako.

kila mmoja anatamani Sana kufanikiwa katika maisha yake, lakini wengi wetu hatujui ni namna gani tunaweza kufanikiwa.

Kwa kutokujua huko ndiko kumetufanya tuendelee kuishi kwa namna ileile na kufanya mambo yaleyale na kwa jinsi ileile miaka nenda miaka rudi na tunashangaa kwa nini maisha yetu hayabadiriki kabisa.

sasa kwa kuwa swala la kutafuta mafanikio siyo jambo rahisi, na kwa kuwa hakuna mafanikio yanayopatikana kwa siku Moja tu kama ajali.

Kupitia Makala hii ninakwenda kukufundisha mambo matatu ambayo unatakiwa kuwa nayo ili uweze kufikia mafanikio ya juu zaidi

ili uweze kufanikiwa unaitaji mambo matatu muhimu na ya msingi ambayo ni

WAZO, WATU NA FEDHA.

Ukiwa na mambo haya matatu na ukayafanyia Kazi kwa bidii kufanikiwa kwako ni uhakika kabisa

ebu tuangalie kwa nini mambo haya ni muhimu Sana kuwa nayo kama kweli unaitaji mafanikio

Jambo la kwanza ni WAZO

Mafanikio yoyote yale yanaanza na mawazo, unapokuwa na wazo juu ya jambo au kitu fulani ndani ya akili yako, jua kwamba hiyo ni roho ya uumbaji wa kitu icho na kinakuwa tayari kimekamilika na kinakuitaji wewe kuweza kukitoa ili kiwe kitu halisi na kinachoonekana ki uhalisia katika dunia.

Mfano ukiwa na wazo kichwani mwako labda wazo la kuanzisha biashara au kufungua kampuni, tayari kampuni au biashara iyo inaishi ndani yako na akili yako imekubali kuwa ndicho kitu unachokiitaji.

Hivyo basi jambo lolote lile linaanza na wazo, kila kitu unachokiona Leo katika dunia hii kilianza na wazo kichwani mwa mtu. Na mtu uyo akaamua kuweka katika utekelezaji na ndiyo maana kikatimia.

Jambo la pili ni WATU.

Kuwa na wazo peke yake hakutoshi unaitaji watu ili kuweza kusaidiana nao kutimiza wazo ulilonalo.

sisi wanadamu tuna ukomo, atuwezi kufanya mambo yote peke yetu na ndiyo maana tunaitaji watu wengine wa kusaidiana nao.

Kuna msemo unasema ukitaka kufika haraka nenda peke yako lakini ukitaka kufika mbali nenda na wenzako.

Hiyo ndiyo nguvu ya lasilimali watu. Kwani watakusaidia kufanya mambo mengi Sana mambo ambayo wewe uwezi kuyafanya mwenyewe labda kwa sababu ya kukosa muda, Ujuzi, fedha na uzoefu.

ukiwa na wazo ukawa na watu mambo yanakuwa mazuri kabisa na unakuwa umepiga hatua Sana katika safari ya kutafuta mafanikio.

Jambo la Tatu ni FEDHA

kuwa na wazo pamoja na watu pekee hakutoshi bado utaitaji kuwa na fedha kwa ajili ya utekelezaji wa wazo lako.

kumbuka mafanikio yoyote yale yana gharama,lazima ujue gharama halisi ya ndoto yako na uwe tayari kulipa gharama izo kama kweli unaitaji kufanikiwa.

ivyo katika mtiririko huu tunaona fedha Inaitajika Sana ili kufanikiwa.

tunaitaji fedha kwa ajili ya mtaji na utekelezaji wa wazo tulilonalo, tunaitaji fedha kwa ajili ya uendeshaji na ulipaji wa matumizi mbalimbali ikiwa ni pamoja na watu tunaosaidiana nao lakini pia matumizi mengine ambayo yanaitajika ili kuweza kufikia mafanikio makubwa.

hivyo basi kwa mafanikio yoyote unayoitaji kuyafikia unatakiwa kuwa na mambo hayo matatu muhimu ambayo ni WAZO, WATU NA FEDHA.

Japo kuwa mambo haya yote ni muhimu Sana kuwa nayo ili kufanikiwa unapaswa kujua kuwa yote hayawezi kuja kwa pamoja. Yaani uwezi kuwa na mambo yote kwa pamoja hasa unapoanza safari yako ya kuelekea kwenye mafanikio.

unaweza ukawa na wazo lakini usiwe na pesa, au ukawa na pesa lakini huna wazo, pia unaweza ukawa na pesa pamoja na wazo lakini ukawa hauna watu.

Anza na utakacho kuwa nacho. Kama utakuwa na wazo tafuta watu wenye pesa shirikiana nao, kama utakuwa na pesa tafuta watu wenye mawazo shirikiana nao na kama hauna pesa na hauna wazo shirikiana na watu kwani pesa na mawazo yote yapo kwa watu wengine kwa kushirikiana nao na wewe unaweza kupata vyote.

Kumbuka mafanikio ni mchakato, na siyo kitu rahisi tu yaani unalala masikini na unaamka tajiri. Kubali kulipa gharama zote uku ukiwa na vitu ivyo vitatu nawe utafanikiwa.

Sijui ni ndoto gani unaitaji kuitimiza maishani mwako?

Amini kuwa inawezekana na kwa hali yoyote uliyonayo anza na kimoja ulichojifunza kwenye SoMo ili.

Mungu akubariki Sana na kukuongoza katika safari yako ya kutafuta mafanikio.

Mimi ninakutamkia mafanikio

Nenda kafanikiwe

asante.


Posted

in

by

Tags:

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *