Hii ndiyo njia ya mkato ya kufikia mafanikio kwa haraka.

Kila mmoja anataka kufikia mafanikio makubwa kwenye maisha yake. Hili linadhihirishwa na jinsi watu wanavyo fanya Kazi kwa bidii Sana wakitafuta pesa zitakazo wasaidia kutimiza maitaji Yao na kuwa na maisha yenye furaha.

licha ya kuwepo kwa njia mbalimbali za kutafuta pesa na mafanikio, bado watu wengi wameshindwa kuzitambua na kuzitumia ili kufanikiwa.

wengi wamekuwa wanakimbizana na fursa chungu nzima zinazoibuka kila siku, wakiamini kuwa kupitia izo watatoboa ki maisha, jambo ambalo si sahihi na limewaliza watu wengi hasa kwa kipindi cha sasa.

kila siku watu wamekuwa wakijiuliza na kutafuta njia za mkato za kufikia mafanikio kwa haraka. Wanaamini kuwa kama wataipata njia iyo basi swala la maisha kwao litakuwa ni bambam na furaha itatawala maisha Yao yote.

kutokana na kuwa watu wengi wamevurugwa na hali za maisha wanayoishi, baadhi ya watu wamekuwa wakitafuta kufanikiwa kwa njia ambazo siyo sahihi.

hapa ndipo utakuta kundi kubwa la watu wana jiingiza katika matendo maovu kama ujambazi, uporaji, wizi, Utekaji wa binadamu, utapeli na kutafuta pesa kwa njia ya udanganyifu.

wengine wamekuwa wakiuza madawa ya kulevya, viungo vya binadamu, biashara za megendo, ufisadi na shughuri hata za uzalilishaji wa kingono.

kuna wengine wanaamini kuwa kufanikiwa mpaka utumie njia za kishirikina kama uchawi na utoaji wa kafara na wamekuwa wanafuata njia izo.

haya yote ni katika utafutaji wa pesa na mafanikio ya haraka.

wengine wameingia kwenye michezo ya bahati nasibu, kamari, na uwekezaji kwenye biashara ambazo hawazijui hasa za mitandaoni. Ikiwa ni katika harakati za kujitafuta na kutafuta njia ya mkato ya kufanikiwa.

Lakini sasa yote hayo bado hayajawa msaada wa kweli kwa watu wengi na hata kwa wale wachache waliotumia njia izo na wakafanikiwa, mafanikio yao huwa hayadumu na mwisho wake wanaishia kwenye majuto na taabu kwa sababu njia walizotumia kupata utajiri na mafanikio hazikuwa sahihi.

Sasa basi kwa kuwa watu wengi wanatafuta njia ya haraka na ambayo ni sahihi kwa wao kuitumia ili kufikia utajiri na mafanikio

Timiza Ndoto Academy ndiyo sehemu sahihi ya wewe kupata njia iyo na kupitia Makala hii ya Leo ninakwenda kukushirikisha njia hiyo ya makato ambayo ukiielewa na kuitumia mafanikio kwako yatakuwa uhakika yaani asilimia 100.

Njia yenyewe ni hii.

TAFUTA WATU WALIO FANIKIWA KATIKA ENEO UNALOTAKA KUFANIKIWA KISHA JIFUNZE KUTOKA KWAO.

Ndugu yangu swala la kutafuta mafanikio halijawai kuwa rahisi Wala Lele mama kama watu wengi wanavyo tegemea.

Na ndiyo maana wanaotafuta mafanikio ni wengi sana lakini waliofanikiwa ni wachache.

Hili ni kutokana na kuwa watu wengi hawajui namna mafanikio yanavyotafutwa na hata kwa wale wanaojua hawajawa tayari kulipa gharama zinazotakiwa ili kupata mafanikio hayo.

Licha ya kuwa swala la kutafuta mafanikio limekuwa ni gumu kwa watu wengi, bado kuna wengi sana wamefanikiwa kuwa na mafanikio makubwa.

kitendo cha watu wengine kufanikiwa kinatupa picha kuwa hata wewe unaweza kufanikiwa kama utakuwa tayari kuwatafuta watu hao na kuwa tayari kujifunza kutoka kwao kuhusu Imani Yao, Tabia zao, njia walizotimia na jinsi walivyofanya mpaka wakafanikiwa na wewe ufanye ivyoivyo.

Kujifunza kutoka kwa walio fanikiwa ndiyo njia ya Makato na ya halali iliyo thibitishwa na inayoweza kukuletea mafanikio kwa haraka kwa sababu watu waliofanikiwa watakusaidia wewe kuepukana na makosa ambayo ungeyafanya kwenye safari yako ya kutafuta mafanikio.

lakini pia watakupa uzoefu wa nini unatakiwa kufanya na ni njia gani ambazo ukizitumia na kuzifuata zitakusaidia kuongeza Kasi zaidi.

pia watakupa muongozo sahihi na Imani sahihi waliyoitumia na kufanikiwa.

Ndugu yangu kama kweli na wewe umechoshwa na hali ya maisha unayoishi sasa na umekuwa ukitumia njia za mkato zisizofaa kutafuta mafanikio yako SoMo hili likusaidie..

….na kwa kuwa sasa umeshajua njia hii ya Makato ya kutafuta mafanikio kwa haraka ni wito wangu kwako kuanza kuitumia njia hii kuanzia sasa ili uweze kufanikiwa.

naamini umejifunza na utaweka katika matendo SoMo ili

Amua sasa chukua hatua na utafanikiwa

Mungu akubariki Sana

nenda kafanikiwe

asante


Posted

in

by

Tags:

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *